Monday 19 June 2017

Marekani yatoa majina ya wanajeshi waliouwawa baharini



The USS Fitzgerald, damaged by colliding with a Philippine-flagged merchant vessel, on 17 June 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionAjali hiyo ilisababisha shimo kubwa kweny meli ya kijeshi
Marekani imetangaza majina ya wanajeshi wake 7 ambao waliuawa wakati meli yao iligongana na ile ya mizigo katika eneo la bahari ya Japan siku ya Jumamosi.
Wanjeshi hao walipatikana katika maneo yaliyokuwa yamefurika maji ndani ya meli hiyo ya kivita ya USS Fitzgerald.
Wanajeshi wengine watatu walijeruhiwa kwenye kisa hicho ambacho kilitokea karibu na mji wa bandari wa Yokosuka.
Meli hiyo kwa sasa imepelekwa huko YokosukaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli hiyo kwa sasa imepelekwa huko Yokosuka
Wengi wa wanajeshi walikuwa wamelala wakati meli hizo ziligongana. Marekani inasema kuwa inafanya uchunguzi.
Wanajeshi hao waliripotiwa kutoweka baada ya ajali hiyo.
Kamanda wa meli ya kijeshi Joseph P Aucoin aliwaambai waandishi wa habari kuwa ajali hiyo ilisababisha shimo kubwa kwenye meli ya kijeshi.
Wanajehsi hao saba ni pamoja na:
  • Dakota Kyle Rigsby, 19
  • Shingo Alexander Douglass, 25
  • Ngoc T Truong Huynh, 25
  • Noe Hernandez, 26
  • Carlos Victor Ganzon Sibayan, 23
  • Xavier Alec Martin, 24
  • Gary Leo Rehm Jr, 37
Map showing location of USS Fitzgerald crash - 17 June 2017
Image captionRamani inayoonyesha eneo la ajali

0 comments:

Post a Comment