Saturday, 10 June 2017

Iringa: Majambazi wajeruhi na kupora fedha na dhahabu katika mgodi

Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia mgodi wa dhahabu wa wachimbaji wadogo katika kijiji cha Nyakavangala kilichopo katika tarafa ya Isimani wilayani Iringa na kupora fedha tasilimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 80 na gramu 400 za dhahabu huku wakiwajeruhi watu tisa.

Majeruhi wa tukio hilo la uporaji ambao baadhi yao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wamesimulia tukio hilo lililotokea siku ya tarehe 9 mwezi huu majira ya saa moja jioni ambapo kundi hilo la watu walivamia mgodini hapo na kuanza kuwasaka watu waliowataja kwa majina na kuwalazimisha baadhi ya wachimbaji kuwaonesha walipo watu hao.

Baadhi ya majeruhi hao wameiomba serikali kujenga kituo cha polisi katika eneo hilo la mgodi ili kuimarisha usalama wakisema kuwa uporaji huo ulifanyika kwa muda mrefu huku kukiwa hakuna msaada wowote kutokana na eneo hilo kutokuwa na kituo cha polisi wala huduma ya mtandao wa simu hali iliyowafanya majambazi hao kufanya tukio hilo kwa muda wa zaidi ya saa kwakuwa walijua hawatabughudhiwa wala kufurushwa na vyombo vya usalama.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka waporaji hao tangu walipopata taarifa hizo hapo jana na kuongeza kuwa serikali inashirikiana na wachimbaji katika eneo hilo la Nyakavangala kuratibu ujenzi wa kituo cha polisi ili kudhibiti usalama wa eneo hilo huku muhudumu wa afya wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Bi Gloria Mnyonge akielezea hali za majeruhi hao.

Related Posts:

  • HIKI HAPA: alichokisema John Bocco Bocco (kulia) akikabidhiwa jezi ya Simba na rais wa klabu hiyo Evans Aveva, imeteka vichwa vya habari vya mitandao mbalimbali ambapo mashabiki wa Simba wameonyesha kufurahishwa na usajili huyo. UONGOZI wa Simba, jana umeta… Read More
  • Mzee Akilimali ataka kumpiku Manji, atangaza kuwania uenyekiti Yanga AKILIMALI Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahimu Akilimali ametangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa klabu ya hiyo iliyoachwa wazi hivi karibuni na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.Hivi karibuni M… Read More
  • AJALI:Gari la polisi laua bodaboda Gari la Polisi MTU mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda waliyokuwa wakitumia kusafiri, kugongana uso kwa uso na gari la Jeshi la Polisi katika wilaya ya Rorya… Read More
  • HALI TETE:Chenge agoma kuzungumza Vigogo waliotajwa katika ripoti ya pili ya kuchunguza makontena yenye mchanga wa madini (makinikia)  kuisababishia Serikali hasara ya matrilioni ya fedha kupitia sekta ya madini, walipokuwa wakihudumu katika nyadhifa … Read More
  • Lissu Amtolea Uvivu JK kuhusu kusaini mikataba ya Madini Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ameitaka Serikali kumjumuisha Rais Mstaafu kwenye tuhuma za Makontena ya Mchenga wa Dhahabu,Akichangia bungeni katika hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18, Lissu am… Read More

0 comments:

Post a Comment