Wednesday, 7 June 2017

Wapelekwa kortini kwa tuhuma za kuiba kanisani

WAKAZI wa wawili wa Ubungo Riverside, Dar es Salaam, Ayubu Sanga (21) na Nafaife Kayinga (19) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kwa tuhuma za kuiba vitu vyenye thamani Sh 1,025,000 katika Kanisa la T.A.G Kinondoni.

Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Ester Kihiyo msoma Mashitaka Dorah Chambo, alidai kwamba washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo mnamo Aprili 16, 2017 majira ya saa saba mchana maeneo ya Kanisa la T.A.G Kinondoni Biafra.

Alidai washitakiwa waliiba mkoba uliokuwa na fedha taslimu Sh 160,000, simu tatu aina Samsung J7, Techno Jpad, Huawei na vitambulisho mbalimbali ikiwemo leseni ya udereva vyote vikiwa na thamani ya Sh 1,025,000 mali ya Doris Mackenzie.

Washitakiwa wote walikana mashitaka hayo na kurudishwa rumande, baada ya kushindwa kutimiza mashariti ya dhamana walipohitajika kila mmoja kuwa na wadhamini wawili, watakaoahidi dhamana ya Sh milioni 2. Kesi hiyo itatajwa tena Juni 13 mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment