Wednesday 7 June 2017

MAANDAMANO:Bobaboda watawanywa kwa mabomu ya machozi

Jeshi la polisi mkoani Shinyinga limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya madereva Bobaboda ambao walikuwa wakiaandamana kuonyesha kupinga kitendo cha polisi baada ya dereva bodaboda mmoja kufariki wakisema kifo chake kimesababishwa polisi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wanasema tukio hili limetokea leo majira ya saa moja asubuhi hadi saa sita mchana ambapo askari polisi walikuwa wakipimana nguvu na bodaboda hao kwa kutupiana mawe na mabomu, hali ambayo ilipelekea kusitisha shughuli za kijamii mjini hapo.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Jumanne Murilo, alisema wameamua kuzuia maandamano hayo kwa sababu yana hatarisha hali ya usalama na maandamano hayo siyo halali, ambapo hawakupaswa kufanya hivyo, bali walitakiwa kutii sheria bila shuruti, na kufuata taratibu za kudai kuonewa, na siyo kutishia kuharibu amani.

"Tumeamua kufanya hivi ili kuzuia kitendo cha watu wachache ambao wametaka kuvuruga amani, kwa kuwapiga mabomu na maji ya kuwasha, ili kuhakikisha utulivu unatawala," alisema Murilo
Hata hivyo jeshi hilo halikuishia hapo , bali lilikwenda hadi nyumbani kwenye msiba alipokuwa akiishi marehemu, na kuutawanya kwa kuwa kamata bodaboda na pikipiki zao hali iliyozua taharuki zaidi.

0 comments:

Post a Comment