Wednesday 7 June 2017

Sudan kumhukumu kifo mwanaharaki wa haki za Binadamu

Mkereketwa wa haki za binadamu, Bw. Sudan Mudawi Ibrahim AdamHaki miliki ya pichaAMNESTY
Image captionMkereketwa wa haki za binadamu, Bw. Sudan Mudawi Ibrahim Adam
Mwanaharakati mmoja maarufu nchini Sudan Bw. Mudawi Ibrahim Adam, angali amesalia ndani ya jela, baada ya kuzuiliwa na wakuu wa nchi hiyo miezi sita iliyopita.
Kufikia sasa hakuna tarehe ambayo imewekwa, ili kusikizwa kwa kesi dhidi yake.
Wanaharakati wa kimataifa, wametoa wito wa kuachiliwa huru kwake mara moja na bila masharti.
Bintiye Wafa, ambaye yuko katika mji mkuu, Khartoum, amemuambia mwaandishi wa BBC James Copnall, kwamba babake anazuiliwa kwa sababu ya kazi zake chini ya shirika la Amnesty International, linalodai kuwa utawala wa Khartoum ulitumia silaha za sumu dhidi ya raia katika maeneo ya magharibi mwa Darfur.
Anasema kuwa, haina ushahidi kumhusisha babake na ripoti hiyo, lakini huenda anazuiliwa kwa kuripoti visa vya ukiukaji wa haki za binadamu katika eneo hilo.

source:bbc

0 comments:

Post a Comment