Watu 8 wamefariki baada ya kimbunga kikali kugonga mji wa Cape Town, Afrika Kusini; upepo mkali ambao vyombo vya Habari vya Afrika Kusini, vimeutaja kama "mama wa vimbunga vyote".
Taasisi zote za elimu zikiwemo vyuo vikuu vimefungwa, huku paa za nyumba na zikifumuliwa na upepo huo mkali.
Manusura wametafutiwa makao mapya mahala salama.
Kimbunga hicho kinagonga baada ya kumalizika kwa ukame mkali wa karne kulikumba taifa hilo.
0 comments:
Post a Comment