Maafisa wa forodha mjini Shanghai nchini China, wanasema kuwa wamemkamata mwanamke ambaye alijaribu kusafirisha mikoba miwili hadi nchini Uchina, ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa kutumia dawa ya kulevya ya cocaine.
Mwezi Februari mamlaka za viwanja vya ndege katika moja ya viwanja vya kimataifa mjini humo zilikagua kwa njia ya x-ray mkoba wa mwanamke ambaye alikuwa amesafiri kutoka nchi ambayo haikutajwa ya Amerika Kusini.
Mashine ya x-ray ilionyesha kuwa mkoba wake ulikuwa mweusi kuliko kawaida na pia ulikuwa mzito hata ulipokuwa bila mzigo.
Baadaye ya uchunguzi uligundua kuwa ulikuwa umetengenezwa kwa karibu kilo kumi ya cocaoine
Sheria za China zinasema kuwa yeyote ambaye atapatikana na hatia ya kusafirisha zaidi ya gramu 50 ya cocaine atanyongwa.
0 comments:
Post a Comment