Kasisi mmoja anayejiita nabii na ambaye alisababisha utata nchini Afrika Kusini, mwaka 2015, baada ya kutuhumiwa kuwafanya watu kula nyoka, panya na nywele ameonekana kwenye ibada nchini Nigeria
Kasi huyo alioneaka katika ibada iliyoongozwa na mhubiri maarufu wa runinga nchini Nigeria TB Joshua mjini Lagos.
Bw. Joshua ameandika katika mtandao wake wa kijamii kumhusu Mchungaji Penuel Mnguni, kuhudhuria ibada yake.
Gazeti la Afrika Kusini, Citizen, limemnukuu Bw. Mnguni akisema kuwa amebadilisha moyo wake, baada ya kujikuta ndani ya utata na habari zake kugonga vichwa vya habari duniani- huku akikamatwa na kuachiwa mara kwa mara:
''Nilianza kutizama runinga ya Emmanuel TV, kumsikiliza nabii TB Joshua, na nikafahamu kuwa, nilichokuwa nikifanya haikuambatana na maandiko. Nilifahamu kuwa lilikuwa shambulio. Nikaja hadi kwa TB Joshua ili anikomboe." Amesema Bw. Mnguni.
Mashtaka dhidi ya Bw. Mnguni, yaliyowasilishwa na chama cha kupambana na dhuluma dhidi ya wanyama (Society for the Prevention of Cruelty to Animals), Afrika Kusini, yaliondolewa mnamo Julai mwaka 2015, kwa kukosa ushahidi.
0 comments:
Post a Comment