Monday, 5 June 2017
Home »
» Jeneza la mwili wa Ndesamburo lazuiwa kupitishwa barabarani
Jeneza la mwili wa Ndesamburo lazuiwa kupitishwa barabarani
Moshi. Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi wa Moshi limezuia utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa kuutembeza katika barabara za viunga vya manispaa hiyo, mwili aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, marehemu Philemon Ndesamburo .
Majibu ya barua yaliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Polisi Moshi, yamezuia mwili huo kupitishwa katika barabara za kati kati ya mji kwa kile walichoeleza kuwa leo Juni 5 na siku ya kazi na kuna shughuli za mbalimbali zinazoendelea.
Sababu ya pili iliyotolewa na ofisi hiyo ni kwamba wakiupitisha mwili huo barabarani watasababisha msongamano mkubwa ambao utakuwa chanzo cha usumbufu kwa watumiaji wengi wa barabarani.
“Ofisi ya Mkuu wa polisi wa wilaya inatoa maelekezo kuwa mwili wa Ndesamburo ukitolewa KCMC, upitishwe barabara ya YMCA kupitia Lucy Lameck Road hadi uwanja wa michezo wa Majengo ambapo kumepangwa kufanyika kwa shughuli zote za kutoa heshima za mwisho.
Jana mmoja wa wanakamati ya mazishi ya Ndesamburo, Anthony Komu aliliambia Mwananchi kuwa mwili wa Ndesamburo utachukuliwa KCMC saa 4 asubuhi na kupitishwa katika barabara kuu za mji wa Moshi ili kuwawezesha ambao hawatapata nafasi ya kufika Majengo, kuuaga mwili huo.
Related Posts:
Jeshi la Polisi Tanzania, latoa onyoImage captionMkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa onyo kwa wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu na kusababisha mauaji ya raia na polisi. Akizungumza kwa mara ya kwan… Read More
Viongozi wa Afrika wamlaumu Trump kuupuza mkataba wa ParisImage captionRais wa zamani wa Ghana John Mahama (pichani) alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa dunia waliounga mkono makubaliano hayo ya kihistoria juu ya mazingira mjini Paris 2015 Rais wa zamani wa Ghana John Mahama amelaan… Read More
Mwanafunzi anayetaka ukasomee Korea KaskaziniImage captionWakati wa kikombe cha chai katika jumba la "urafiki wa kimataifa" Korea Kaskazini inapotajwa, linalotokea akilini mwa wengi sana huwa ni majaribio ya makombora na silaha za nyuklia, pamoja na kiongozi wake Kim Jo… Read More
Obama anunua nyumba ya $8.1m ya kuishi Washington DCHaki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMali ya Obama ikihamishiwa Washinton baada yake kuondoka White House mwezi Januari Familia ya Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama imenunua nyumba ambayo kwa muda wamekuwa wakiish… Read More
Ufilipino: Watu 36 wafariki chumba cha kamari ManilaHaki miliki ya pichaEPAImage captionKituo cha kamari cha Resorts World Manila kimewekwa chini ya ulinzi mkali baada ya kisa hicho Watu 36 wameuawa katika kituo cha kuchezea kamari mjini Manila, Ufilipino baada ya mtu mwenye s… Read More
0 comments:
Post a Comment