Msanii Chipukizi kutoka Mdee music 'Mimi Mars' mwenye 'hit' mpya inayokwenda kwa jina la 'Dede' amefunguka na kusema dada yake Vanessa Mdee ni mtu ambaye hawezi kushaurika kuhusu mavazi pindi anapokuwa amepangilia kuvaa.
Vanessa Mdee kushoto, Mimi Mars kulia
Mimi Mars ambaye ni mdogo wa msanii Vanessa Mdee amesema kuwa mara kadhaa mavazi ya dada ake yanayomkwaza huwa anamuambia lakini majibu anayopatiwa yanamfanya ashindwe kuendelea kuhoji na kushauri.
"Inapotokeaga amevaa nguo ambayo sijaipenda namuulizaga Mamdogo hiyo nguo vipi? lakini atakuambia eeeh fashion babu niache napanda zangu stejini, so nakua i'm like ok, hivyo ikifika hapo nakuwa siwezi tena kumshauri . Yeye ni Icon na 'Star' hivyo labda wakati mwingine huwa anapenda kuwa na aina fulani ya muonekano stejini hivyo ni vigumu sana kumbadilisha - Mimi Mars
Kwa upande wake Mimi Mars ameweka wazi hataweza kuvaa nguo kama za dada yake hata kwenye video zake za muziki kwa vile hana mwili unamruhusu kujiachia kama dada yake.
Mwili wa Mzee Francis Maige Kanyasu alimaarufu kwa jina la Mzee Ngosha ambaye anayetajwa kuwa ni moja wa wachoraji wa nembo ya Taifa aliyefariki tarehe 30 mwezi wa 5 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili. unatarajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Misungwi Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Maendeleo ya Jamii) imesema kuwa ndugu wa Mzee Kanyasu wamepatikana na sasa serikali itagharamia kusafirisha mwili wa mzee huyo mpaka Mwanza ambapo atakwenda kuzikwa huko.
Mwili wa Mzee Francis Maige unatarajiwa kuagwa kesho Jumamosi saa 2 asubuhi Hospitali Taifa ya Muhimbili kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza.
Haki miliki ya pichaTHINKSTOCKImage captionKuwepo kwa TV katika chumba cha kulala cha mtoto kunaweza kumsababishia kutopata usingizi wa kutosha na kuwa na tabia ya ulaji usiofaa
Watoto wenye TV katika vyumba vyao vya kulala wana uwezekano mkubwa wa kuwa na uzito wa kupindukia kuliko wale ambao hawana, utafiti katika chuo cha wanasayansi cha London London kinasema.
Watafiti walibaini kuwa watoto wasichana kadri wanavyokaa muda mrefu wakitazama TV, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano mkubwa wa uzito wao wa mwili kuongezeka.
Watafiti wanasema kuna haja ya haraka sasa ya kuchunguza uwezekano huo kwa watumiaji wa vipakatanishi (laptops) na simu za mkononi (mobiles).
Wataalam wanasema wakati watoto wanapotumia muda mefu kutazama TV hupata madhara mengi ya kiafya.
Utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la Kimataifa kuhusu Unene wa kupindukia (International Journal of Obesity) ulitathmini data kutoka kwa watoto wadogo zaidi ya 12,000 nchini Uingereza.
Wanasayansi hao walibaini kuwa zaidi ya nusu ya watoto waliokuwa na TV katika vyumba vyao vya kulala wakiwa na umri wa miaka saba.
Wazazi waliulizwa kueleza ni kwa kiwango cha saa ngapi kwa siku watoto wao hutazama TV kwa ujumla .
Baadae , watoto hao walipofikia umri wa miaka 11, watafiti walipima viwango vya uzito wao wa mwili kulingana na kimo chao cha urefu kwa kuangalia asilimia ya mafuta ya mwili waliyonayo.
Wasichana waliokuwa na TV ndani ya vyumba vyao vya kulalawakiwa na umri wa miaka saba walipatikana na asilimia 30% ya uwezekano wa kuwa na uzito wa mwili wa kupindukia wanapofika umri wa miaka 11, wakilinganishwa na watoto wenzao ambao hawakuwa na TV vyumbani mwao.
Kwa wavulana, hatari hiyo iliongezeka kwa asilimia 20%.
Mtafiti Dr Anja Heilmann, alisema: "utafiti wetu unaonyesha kuwa kwamba kuna ushahidi wa wazi wa uhusiano baina ya kuwana TV chumbani kwa mtoto na kuongezeka kwa uzito wa mwili kwa mtoto miaka michache baadae."
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionWatafiti wanajiuliza ikiwa matumizi ya simu za mkononi (mobiles) pia yana uhusiano na kuongezeka kwa unene wa mwili wa kupindukia
Watafiti wanasema hawawezi kuwa na uhakika juu ya nini kinachosababisha uhusiano baina ya kutazama TV na kuongezeka kwa mwili, lakini wanasema huenda sababu ikawa ni watoto wenye TV vyumbani kusinzia kwa muda mfupi wakitumia muda mrefu kuitazama katika vyumba vyao vya kulala ama ulaji wa kiholela wanapotazama TV.
Watafiti wanatoa wito wa kuandaliwa kwa mikakati ya uzuwia unene wa kupindukia miongoni mwa watoto kwa kuangalia njia za kukabliana na tatizo hili.
Katika waraka wao kwenye jarida, wanasema : "wakati screen za TV zikiendelea utengenezwa kuwa vyembamba zaidi, watoto wetu wanakuwa na unene zaidi ."
tabia ya Ulaji usiofaa
Na kuna baadhi ya matokeo ya uchunguzi yaliyobaini kuwepo kwa uhusiano baina ya muda wasichana wanaoketi mbele ya TV na kuongezeka kwa uzito wa mwili husababishw ana kwamba wasichana hufanya mazoezi ya mwili kidogo kuliko wavulana wenye umri sawa na wao.
Profesa Russell Viner, kutoka chuo cha tiba na afya ya watoto cha Royal College (RCPCH) anasema matokeo ya utafiti huo yanapaswa kuchukuliwa kwa umakini zaidi.
Prof Viner anasema utafiti huo unaunga mkono haja ya kuzuwia ulaji wa vyakula visivyo na virutubisho vya mwili pamoja na matangazo ya TV yanayonadi vyakula hivyo
Haki miliki ya pichaAFPImage captionWatoto wa Sudan kusini
Serikali ya Sudan kusini imesema watoto wapatao 15 wakufa ikiwa ni matokeo ya makosa yaliyofanyika katika jaribio la kuwakinga na surua.
Wafanyakazi wa afya katika jimbo la mashariki Ikweta walirudia tena kutumia sindano zisizo na usafi kuwachanja watoto wote.
Waziri wa Afya wa Sudan kusini Riek Gai Kok amesema timu iliyohusika katika kampeni hiyo ya chanjo haikuwa na vigezo wala kupata mafunzo kwa kazi hiyo.
Huduma za afya zimekuwa zikifanya kazi kwa shida Sudan kusini toka kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza mwaka 2013.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionBale na Isco wakitaniana wakati wa mazoezi, mmoja wao huenda atakosa nafasi ya kucheza
Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane anakabiliwa na kizungumkuti cha kuamia nani kati ya Gareth Bale na Isco atacheza katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumamosi.
Bale hajacheza tangu 23 Aprili lakini sasa yuko sawa kucheza.
Isco, ambaye alijaza pengo lake naye amekuwa akicheza vyema sana na amefunga mabao matano katika mechi nane walizocheza hivi karibuni.
"Wote wawili ni wachezaji muhimu sana na kila mmoja anaweza kutoa maoni yake lakini hilo halitaniathiri," Zidane amesema.
Mkufunzi wa Juventus Max Allegri wachezaji wake wote pia wako sawa kucheza.
Gianluigi Buffon, Giorgio Chellini, Alex Sandro, Mario Mandzukic na Leonardo Bonucci walipumzishwa mechi ya mwisho ya Juve katika Serie A dhidi ya Bologna Jumamosi iliyopita.
Gianluigi Buffon, 39, atakuwa nahodha wa Juve katika mechi hiyo itakayochezewa Cardiff.
Buffon hajawahi kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
"Itakuwa na maana kubwa sana kwangu," anasema mchezaji huyo, ambaye amechezea Italia mechi 168.
"Itakuwa siku ya furaha zaidi kwangu katika maisha yangu ya uchezaji, pamoja na Kombe la Dunia - kwa sababu itakuwa ni kama zawadi, baada ya safari ngumu yenye dhiki na visiki na bidii."
Juventus walilaza Monaco 4-1 na kufika fainali kwa mara ya pili katika misimu mitatu.
Real Madrid nao waliwatoa Atletico kwa ushindi wa jumla wa 4-2.
Ronaldo, ambaye alifunga penalti ya ushindi fainali msimu uliopita, anasema amepumzika vya kutosha na ako makini kabisa.
"Mwisho wa msimu ni muhimu sana," anasema.
Ronaldo alifikia magoli 400 ambayo amefungia Real msimu wa sasa, pamoja na mabao 100 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Haki miliki ya pichaPAImage captionUsalama utaimarishwa kwa ajili ya fainali
Hii itakuwa mechi ya 19 kwa klabu hizo mbili kukutana, mechi zote zikiwa katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya.
Klabu hizo ndizo zilizokutana mara nyingi kabisa historia ya michuano hiyo, baada ya Bayern dhidi ya Real Madrid (24).
Juventus na Real Madrid, kila mmoja ameshinda mechi nane kati ya hizo, mechi mbili zikimalizika kwa sare.
Mechi yao pekee kukutana fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Real walishinda 1-0 mwaka 1998 kupitia bao la Pedrag Mijatovic.
Juventus wameshinda mara mbili pekee kati ya fainali nane walizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya. Walishindwa fainali nne walizocheza karibuni zaidi mwaka 1997, 1998, 2003 na 2015.
Real Madrid wanapigania kuwa klabu ya kwanza tangu AC Milan (1989, 1990) kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya misimu miwili mfululizo.
Mwaka huu ni mara ya tatu kwa Real Madrid kufika fainali katika misimu minne.
Juve ndiyo klabu pekee ambayo haijashindwa mechi yoyote msimu huu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, klabu ya kwanza tangu Atletico Madrid mwaka 2013/14 kufika fainali bila kushindwa.
Real Madrid nao wamefunga kila mechi kati ya mechi 12 walizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu.
Haki miliki ya pichaRYAN HARTImage captionClaire na Charlotte Hart
Makaka wawili ambao baba yao alimuua mama yao kwa risasi wamemuelezea baba yao kama "gaidi".
Lance Hart, mwenye umri wa miaka 57, alimuua mkewe Claire, aliyekuwa na umri wa miaka 50, pamoja na binti yao Charlotte, aliyekuwa na miaka 19, kando ya dimbwi la kuogelea (swimming pool) huko Spalding mwezi Julai mwaka jana.
Watoto wake wa kiume, Luke na Ryan, wanasema walihangaika katika maisha yao yote kuvumilia mwenendo wake wa kupenda kudhibiti kila kitu .
" Hakuwa na jambo la maana la kumfanya aishi kuliko kutuua ," alikieleza kipindi cha Victoria Derbyshire Luke, mwenye umri wa miaka 27.
Mauaji hayo yalitokea siku kadhaa baada ya Bi Hart kuondoka katika nyumba ya familia kufuatia mfarakano baina ya wanandoa hao.
Hart aliwapiga risasi mke na binti yake katika eneo la dimbwi la kuogelea karibu na eneo la kuegeshea magari kabla ya kujigeuzia bunduki mwenyewe na kujimiminia risasi zilizomuua.
Luke alisema kuwa lilikuwa ni tendo la mwisho la baba yao kuhakikisha familia haiwezi kuishi bila yeye.
Aliacha waraka wa kurasa 12 akisema "kisasi ni chakula baridi kinachogawiwa kwa walaji ".
" Mtu kama baba yetu alikuwa gaidi. Alikuwa anapanga kutuua sote watatu wiki tatu kabla ya kuwauwa ," Alisema Luke.
" Inapokuwa ni baba yako ... hasira huwa isiyoweza kuelezeka. Ni suala gumu sana na la kutisha na vyombo vya habari vililichukulia tukio hilo kama la kawaida, lakini kwetu lilikuwa ni tatizo lililotusumbua kwa muda mrefu ."
Makaka hao wawili walisema kuwa baba yao alidhibiti nyumba yao kwa kuweka masharti makali ya matumizi ya pesa na kumzuwia mama yao kupata usaidizi wowote wa kijamii.
"alikuwa na namna ya kukufanya ujihisi mnyonge, mtu wa kuhurumiwa na dhaifu na kuhisi unahitaji kusaidiwa ," Alisema Luke.
"alikuwa na utamaduni wa imani kuwa mwanamume ndiye anayeweza kila kitu na watu wengi wanafikiri ni jambo la kawaida.
Alifikiri anatumiliki na alituona kama sisi ni watu wa kulindwa na yeye ."
Luke anasema mama yao alikuwa na kumbu kumbu ya kila kitu ambacho baba yao alikuwa akikisema na kukifanya , lakini "kwa kuwa hapakuwa na ushahidi wa madhara yoyote" hawakudhani kuwa kulikuwa na kitu ambacho wanaweza kukipeleka polisi.
"Hata kama tungefanya hivyo, wangefanyaje? Polisi wangemtoa nje ya nyumba?.
Suala ni kwamba unaweza kuwalinda watu tu kwa kuwafanya wawe na imani ya jumla ya jamii."
Vijana hao , ambao walifanya kazi kwa bidii kuwapatia mama na dada yao maisha bora waliishia kumuondoa ndani ya nyumba yao "ili awe salama " wakati baba yao na mama yao walipoachana.
Wakati wa mauaji hayo, baadhi ya ripoti ziliwanukuu majirani wakimuelezea baba yao -Hart kama "mwanaume mzuri sana sana " ambaye alihangaika kukabiliana na kuvunjika kwa ndoa yake.
Ryan, mwenye umri wa miaka 26, alisema: "kile ambacho magazeti mengi yaliandika juu baba yangu ni kwamba alikuwa mtu mwema na hata kutaka kutetea kile alichokifanya. Si kuhusu maisha ya mama na Charlotte, ila kumuhurumia yeye.
"Pale mateso ya hisia yanapoongelewa muathiriwa husahaulika. Hakuna aina nyingine ya mauaji ambapo muathiriwa hulaumiwa ''
Image captionWakati wa kikombe cha chai katika jumba la "urafiki wa kimataifa"
Korea Kaskazini inapotajwa, linalotokea akilini mwa wengi sana huwa ni majaribio ya makombora na silaha za nyuklia, pamoja na kiongozi wake Kim Jong-un.
Aidha, mara kwa mara taarifa za raia wa nchi za Magharibi kukamatwa na kufungwa jela huripotiwa.
Lakini sasa kuna mwanafunzi Mwingereza ambaye anaamini wengi hawajalifahamu vyema taifa hilo.
Badala ya kuitenga Korea Kaskazini, anaamini wakati umefika kwa watu kufanya urafiki na taifa hilo.
"Tumekuwa wepesi wa kuibandika Korea Kaskazini manenokama vile 'marufuku' 'taifa lenye usiri mkubwa', 'dhiki', 'ukatili' na kadhalika, lakini nataka kuondoa dhana hiyo, angalau kwa dakika moja, tuitazame Korea Kaskazini katika ngazi ya utu,2 anasema Benjamin Griffin, 24.
Kabla yake kufanya ziara yake ya kwanza nchini humo miaka minne iliyopita, ufahamu wake kuhusu nchi hiyo anasema ulitokana na "makala moja pekee aliyokuwa ameitazama na video fupi za YouTube."
Lakini alipata nafasi ya kusafiri taifa hilo kwa kutumia shirika lakitalii la Juche Travel Services (JTS), safari iliyomfumbua macho.
"Nilipoiona Pyongyang kwa mara ya kwanza mwaka 2013, nilitarajia kuwaona wanajeshi kila nilikoenda. Ni kana kwamba sikuwa nawatazama kama watu halisi," anasema.
Lakini ukweli ni kwamba tuliwaona watu wakitembea kwenda kazini, kwenda madukani na kucheza ngoma katika bustani. Kwa kiasi fulani, nilishangazwa na maisha hayo ya kawaida.
"Ukweli ni kwamba, katika maisha ya kila siku ya raia wa Pyongyang, huwa hawana wasiwasi kuhusu njia gani bora ya kukabiliana na ubabe wa Marekani au maovu ya mfumo wa ubepari. Wanachokijali zaidi ni, 'Nitaenda wapi dukani kununua bidhaa? Nimefikia wapi katika kazi yangu? Binti yangu ataolewa?"
Mwaka uliofuata, akiwa na miaka 21, aliyejea huko kama mwalimu wa kujitolea wa somo la Kiingereza katika chuo cha utalii cha Pyongyang.
Baadaye, alihitimu na kuwa mwelekezi wa watalii wa TJS na sasa ameanzisha mpando wa kuwasaidia watu kila tabaka au asili wanaotaka kwenda kukaa chuo kikuu cha Kim Il-sung mwezi Julai.
Washiriki watalala katika mabweni ya chuo na kujifunza Kikorea kwa saa nne kila siku.
Muda huo mwingine watautumia kwa kutembea kujionea mji na vivutio mbalimbali, na kisha kushiriki katika shughuli mbalimbali kama vile kuogelea, kucheza ngoma asili na kucheza mchezo wa kandadna wa wachezaji watano kila upande.
Kutakwua pia na fursa ya kukutana na baadhi ya raia wa Korea Kaskazini, ingawa raia hao watakwua wamechunguzwa kikamilifu.
"Hatuwezi kamwe kusahau matatizo yaliyopo Korea Kaskazini, lakini tunafaa kwua na uelewa fulani. Utalii wa elimu unasaidia hilo.
"Sitaki kuacha kuuliza mazwali lakini ni muhimu pia kuifahamu nchi hiyo kikamilifu, watu wake na thamani na maadili yao.
"Ni kweli kuna siasa - wana majaribio yao ya silaha za nyuklia, na ukiukabi wa haki za kibinadamu - lakini ni muhimu kuangazia uhusiano wa binadamu mmoja na mwingine."
Haki miliki ya pichaEPAImage captionKituo cha kamari cha Resorts World Manila kimewekwa chini ya ulinzi mkali baada ya kisa hicho
Watu 36 wameuawa katika kituo cha kuchezea kamari mjini Manila, Ufilipino baada ya mtu mwenye silaha kuanza kuwafyatulia risasi watu waliokuwemo humo.
Wengi wa waliofariki inaaminika wamefariki kutokana na kukosa hewa safi kutokana na moshi uliotanda mwanamume huyo alipowasha moto meza za chumba hicho cha kamari.
Mwanamume huyo alianza kwa kupiga risasi skrini za TV katika chumba hicho cha Resorts World Manila mapema Ijumaa.
Polisi wanasema baadaye alijiteketeza.
Kisa hicho kimesababisha kuanzishwa kwa operesheni kali ya kiusalama.
Maafisa awali walisema hakuna aliyekwua ameumia kutokana na kisa hicho, lakini sasa inabainika kwamba wamepataa miili ya watu wakikagua chumba hicho.
Polisi wanasema kisa hicho kinaonekana kuwa kisa cha kawaida tu cha wizi, na kwamba hakikuhusiana na ugaidi.
Watu zaidi ya 50 wamepelekewa hospitalini wakiuguza majeraha.
Haki miliki ya pichaPHILIPPINE POLICEImage captionMwanamume huyo alionekana kwenye kamera za CCTV ndani ya chumba hicho
Shambulio lilitekelezwa vipi?
Maafisa wanasema mwanamume huyo, ambaye jina lake halijatajwa kufikia sasa, aliingia ukumbi wa kituo hicho na kuanza kufyatulia risasi skrini za runinga mwendo wa saa sita usiku. Watu waliokuwemo ndani walianza kukimbia.
Pia alichoma moto meza za kamari na kujaza mkoba wake na vipande vya kuchezea kamari vya thamani ya peso milioni 113 za Ufilipino (£1.7m, $2.3m).
Baadaye alikimbia na kuingia upande wa kituo hicho wenye hoteli, akaacha mkoba wake, na kuingia chumba cha hoteli.
"Humo, alilala kitandani, akajifunika kwa blanketi aliyokuwa ameimwagilia mafuta ya petroli na kisha akajiwasha moto," mkuu wa polisi wa taifa Ronald Dela Rosa alisema Ijumaa.
Resorts World Manila wamesema katika taarifa kwamba alijipiga risasi kabla ya kujiwasha moto, na kwamba alipatikana akiwa amefariki mwendo wa saa moja asubuhi saa za Ufilipino.
Maafisa wanasema taarifa zinaonesha mwanamume huyo alikuwa na matatizo ya kiakili.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMali ya Obama ikihamishiwa Washinton baada yake kuondoka White House mwezi Januari
Familia ya Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama imenunua nyumba ambayo kwa muda wamekuwa wakiishi kwa kukodisha mjini Washington DC.
Nyumba hiyo yenye vyumba tisa inapatikana katika mtaa wa kifahari wa Kalorama na iliuzwa $8.1m (£6.2m).
Obama ameamua kuendelea kukaa Washington na familia yake hadi binti yake mdogo, Sasha ambaye ana umri wa miaka 15, amalize masomo ya shule ya upili.
Kiongozi huyo na mkewe Michelle wamekuwa wakizuru mataifa mbalimbali duniani tangu walipoondoka White House mwezi Januari.
Msemaji wa Bw Obama, Kevin Lewis, alithibitisha ununuzi huo na kusema: "Ikizingatiwa kwamba Rais na Bi Obama watakuwa Washington kwa angalau miaka mingine miwili unusu, ina umuhimu kwao kununua nyumba badala ya kuendelea kukodi."
Kuna vizuizi vya saruji kuzuia watu kufikia nyumba hiyo yenye ukubwa wa futi mraba 8,300 (mita mraba 770), ambayo inalindwa saa 24 kila siku na maafisa wa kikosi cha kulinda marais Marekani.
Familia ya Obama bado inamiliki nyumba Chicago.
Walinunua nyumba hiyo kutoka kwa aliyekuwa afisa wa habari wa Bill Clinton Joe Lockhart, aliyeinunua mwaka 2014 kwa $5.3m.
Nyumba hiyo haiko mbali sana na nyumba ya thamani ya $23m inayomilikiwa na mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos, ambaye pia humiliki gazeti la Washington Post.
Bintiye Rais Donald Trump, Ivanka, na mumewe Jared Kushner ambaye kwa sasa ni mshauri mkuu White House, pia wanaishi hapo karibu.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ni afisa mwingine wa ngazi ya juu anayeishi Kalorama, katika nyumba aliyoinunua kwa $5.6m Februari.
Image captionRais wa zamani wa Ghana John Mahama (pichani) alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa dunia waliounga mkono makubaliano hayo ya kihistoria juu ya mazingira mjini Paris 2015
Rais wa zamani wa Ghana John Mahama amelaani uamuzi wa rais wa Marekakani , Donald Trump kwa kuiondoa Marekani kwenye makataba wa Paris wa 2015 kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.
Bwana Mahama alituma ujumbe wake kwa njia ya Twitter, akiutaja uamuzi wa rais Trump wa kujiondoa kwenye makataba huo wa mazingira kama " jambo ambalo ni vigumu kuliamini". ''Ni siku ya huzuni sana katika ushirikiano wa kimataifa ". Uliandikwa ujumbe huo wa Bwana Mahama.
Rais huyo wa zamani wa Ghana alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa dunia waliunga mkono makubaliano hayo ya kihistoria juu ya mazingira mjini Paris, akiahidi kutekeleza hatua za kupunguza hewa ya makaa duniani.
AliTwitt wamba Marekani imejiondoa katika uongozi wake wa dunia.
Bwana Trump alisema kuwa mkataba huo "uliiadhibu" Marekani na utasababisha kupotea kwa mamilioni ya ajira nchini Marekani.
Wakati huo huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Afrika amesema: ''Mabadiliko ya hali ya hewa ni tisho kubwa la enzi yetu, Makubaliano ya Paris ni matokeo ya makubaliano mengi ya ushirikiano na utashi wa kutafuta suluhu ya pamoja ya tatizo la dunia.
Hakuna nchi moja inayoweza kuvuruga makubaliano. Wakati Marekani inajiondoa inadhoofisha mkataba huo wa kimataifa, haitauvunja " Alisema Bwana Annan.
''Kilichosalia kwa mkataba wa Paris ni kwa pande zilizosalia kuendelea kujitolea kuongeza juhudi za kutatua matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi''.Wajumbe wa Baraza la Wazee wa Afrika wanasema .
Ndani ya Marekani kwenyewe, biashara na mamlaka za majimbo zinaweza na lazima zikchukue hatua pale serikali ya shirikisho itakaojiondoa , waliongeza.