Friday 2 June 2017

Ndugu wawili Marekani wasema baba yao aliyemuua mama yao alikuwa ''gaidi''

Claire na Charlotte HartHaki miliki ya pichaRYAN HART
Image captionClaire na Charlotte Hart
Makaka wawili ambao baba yao alimuua mama yao kwa risasi wamemuelezea baba yao kama "gaidi".
Lance Hart, mwenye umri wa miaka 57, alimuua mkewe Claire, aliyekuwa na umri wa miaka 50, pamoja na binti yao Charlotte, aliyekuwa na miaka 19, kando ya dimbwi la kuogelea (swimming pool) huko Spalding mwezi Julai mwaka jana.
Watoto wake wa kiume, Luke na Ryan, wanasema walihangaika katika maisha yao yote kuvumilia mwenendo wake wa kupenda kudhibiti kila kitu .
" Hakuwa na jambo la maana la kumfanya aishi kuliko kutuua ," alikieleza kipindi cha Victoria Derbyshire Luke, mwenye umri wa miaka 27.
Mauaji hayo yalitokea siku kadhaa baada ya Bi Hart kuondoka katika nyumba ya familia kufuatia mfarakano baina ya wanandoa hao.
Hart aliwapiga risasi mke na binti yake katika eneo la dimbwi la kuogelea karibu na eneo la kuegeshea magari kabla ya kujigeuzia bunduki mwenyewe na kujimiminia risasi zilizomuua.
Luke alisema kuwa lilikuwa ni tendo la mwisho la baba yao kuhakikisha familia haiwezi kuishi bila yeye.
Aliacha waraka wa kurasa 12 akisema "kisasi ni chakula baridi kinachogawiwa kwa walaji ".
" Mtu kama baba yetu alikuwa gaidi. Alikuwa anapanga kutuua sote watatu wiki tatu kabla ya kuwauwa ," Alisema Luke.
" Inapokuwa ni baba yako ... hasira huwa isiyoweza kuelezeka. Ni suala gumu sana na la kutisha na vyombo vya habari vililichukulia tukio hilo kama la kawaida, lakini kwetu lilikuwa ni tatizo lililotusumbua kwa muda mrefu ."
Makaka hao wawili walisema kuwa baba yao alidhibiti nyumba yao kwa kuweka masharti makali ya matumizi ya pesa na kumzuwia mama yao kupata usaidizi wowote wa kijamii.
"alikuwa na namna ya kukufanya ujihisi mnyonge, mtu wa kuhurumiwa na dhaifu na kuhisi unahitaji kusaidiwa ," Alisema Luke.
"alikuwa na utamaduni wa imani kuwa mwanamume ndiye anayeweza kila kitu na watu wengi wanafikiri ni jambo la kawaida.
Alifikiri anatumiliki na alituona kama sisi ni watu wa kulindwa na yeye ."
Luke anasema mama yao alikuwa na kumbu kumbu ya kila kitu ambacho baba yao alikuwa akikisema na kukifanya , lakini "kwa kuwa hapakuwa na ushahidi wa madhara yoyote" hawakudhani kuwa kulikuwa na kitu ambacho wanaweza kukipeleka polisi.
"Hata kama tungefanya hivyo, wangefanyaje? Polisi wangemtoa nje ya nyumba?.
Suala ni kwamba unaweza kuwalinda watu tu kwa kuwafanya wawe na imani ya jumla ya jamii."
Vijana hao , ambao walifanya kazi kwa bidii kuwapatia mama na dada yao maisha bora waliishia kumuondoa ndani ya nyumba yao "ili awe salama " wakati baba yao na mama yao walipoachana.
Wakati wa mauaji hayo, baadhi ya ripoti ziliwanukuu majirani wakimuelezea baba yao -Hart kama "mwanaume mzuri sana sana " ambaye alihangaika kukabiliana na kuvunjika kwa ndoa yake.
Ryan, mwenye umri wa miaka 26, alisema: "kile ambacho magazeti mengi yaliandika juu baba yangu ni kwamba alikuwa mtu mwema na hata kutaka kutetea kile alichokifanya. Si kuhusu maisha ya mama na Charlotte, ila kumuhurumia yeye.
"Pale mateso ya hisia yanapoongelewa muathiriwa husahaulika. Hakuna aina nyingine ya mauaji ambapo muathiriwa hulaumiwa ''

0 comments:

Post a Comment