Friday 2 June 2017

Mwanafunzi anayetaka ukasomee Korea Kaskazini

Chai
Image captionWakati wa kikombe cha chai katika jumba la "urafiki wa kimataifa"
Korea Kaskazini inapotajwa, linalotokea akilini mwa wengi sana huwa ni majaribio ya makombora na silaha za nyuklia, pamoja na kiongozi wake Kim Jong-un.
Aidha, mara kwa mara taarifa za raia wa nchi za Magharibi kukamatwa na kufungwa jela huripotiwa.
Lakini sasa kuna mwanafunzi Mwingereza ambaye anaamini wengi hawajalifahamu vyema taifa hilo.
Badala ya kuitenga Korea Kaskazini, anaamini wakati umefika kwa watu kufanya urafiki na taifa hilo.
"Tumekuwa wepesi wa kuibandika Korea Kaskazini manenokama vile 'marufuku' 'taifa lenye usiri mkubwa', 'dhiki', 'ukatili' na kadhalika, lakini nataka kuondoa dhana hiyo, angalau kwa dakika moja, tuitazame Korea Kaskazini katika ngazi ya utu,2 anasema Benjamin Griffin, 24.
Kabla yake kufanya ziara yake ya kwanza nchini humo miaka minne iliyopita, ufahamu wake kuhusu nchi hiyo anasema ulitokana na "makala moja pekee aliyokuwa ameitazama na video fupi za YouTube."
Lakini alipata nafasi ya kusafiri taifa hilo kwa kutumia shirika lakitalii la Juche Travel Services (JTS), safari iliyomfumbua macho.
"Nilipoiona Pyongyang kwa mara ya kwanza mwaka 2013, nilitarajia kuwaona wanajeshi kila nilikoenda. Ni kana kwamba sikuwa nawatazama kama watu halisi," anasema.
Lakini ukweli ni kwamba tuliwaona watu wakitembea kwenda kazini, kwenda madukani na kucheza ngoma katika bustani. Kwa kiasi fulani, nilishangazwa na maisha hayo ya kawaida.
"Ukweli ni kwamba, katika maisha ya kila siku ya raia wa Pyongyang, huwa hawana wasiwasi kuhusu njia gani bora ya kukabiliana na ubabe wa Marekani au maovu ya mfumo wa ubepari. Wanachokijali zaidi ni, 'Nitaenda wapi dukani kununua bidhaa? Nimefikia wapi katika kazi yangu? Binti yangu ataolewa?"
Mwaka uliofuata, akiwa na miaka 21, aliyejea huko kama mwalimu wa kujitolea wa somo la Kiingereza katika chuo cha utalii cha Pyongyang.
Baadaye, alihitimu na kuwa mwelekezi wa watalii wa TJS na sasa ameanzisha mpando wa kuwasaidia watu kila tabaka au asili wanaotaka kwenda kukaa chuo kikuu cha Kim Il-sung mwezi Julai.
Washiriki watalala katika mabweni ya chuo na kujifunza Kikorea kwa saa nne kila siku.
Muda huo mwingine watautumia kwa kutembea kujionea mji na vivutio mbalimbali, na kisha kushiriki katika shughuli mbalimbali kama vile kuogelea, kucheza ngoma asili na kucheza mchezo wa kandadna wa wachezaji watano kila upande.
Kutakwua pia na fursa ya kukutana na baadhi ya raia wa Korea Kaskazini, ingawa raia hao watakwua wamechunguzwa kikamilifu.
"Hatuwezi kamwe kusahau matatizo yaliyopo Korea Kaskazini, lakini tunafaa kwua na uelewa fulani. Utalii wa elimu unasaidia hilo.
"Sitaki kuacha kuuliza mazwali lakini ni muhimu pia kuifahamu nchi hiyo kikamilifu, watu wake na thamani na maadili yao.
"Ni kweli kuna siasa - wana majaribio yao ya silaha za nyuklia, na ukiukabi wa haki za kibinadamu - lakini ni muhimu kuangazia uhusiano wa binadamu mmoja na mwingine."

0 comments:

Post a Comment