Watoto wenye TV katika vyumba vyao vya kulala wana uwezekano mkubwa wa kuwa na uzito wa kupindukia kuliko wale ambao hawana, utafiti katika chuo cha wanasayansi cha London London kinasema.
Watafiti walibaini kuwa watoto wasichana kadri wanavyokaa muda mrefu wakitazama TV, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano mkubwa wa uzito wao wa mwili kuongezeka.
Watafiti wanasema kuna haja ya haraka sasa ya kuchunguza uwezekano huo kwa watumiaji wa vipakatanishi (laptops) na simu za mkononi (mobiles).
Wataalam wanasema wakati watoto wanapotumia muda mefu kutazama TV hupata madhara mengi ya kiafya.
Utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la Kimataifa kuhusu Unene wa kupindukia (International Journal of Obesity) ulitathmini data kutoka kwa watoto wadogo zaidi ya 12,000 nchini Uingereza.
Wanasayansi hao walibaini kuwa zaidi ya nusu ya watoto waliokuwa na TV katika vyumba vyao vya kulala wakiwa na umri wa miaka saba.
Wazazi waliulizwa kueleza ni kwa kiwango cha saa ngapi kwa siku watoto wao hutazama TV kwa ujumla .
Baadae , watoto hao walipofikia umri wa miaka 11, watafiti walipima viwango vya uzito wao wa mwili kulingana na kimo chao cha urefu kwa kuangalia asilimia ya mafuta ya mwili waliyonayo.
Wasichana waliokuwa na TV ndani ya vyumba vyao vya kulalawakiwa na umri wa miaka saba walipatikana na asilimia 30% ya uwezekano wa kuwa na uzito wa mwili wa kupindukia wanapofika umri wa miaka 11, wakilinganishwa na watoto wenzao ambao hawakuwa na TV vyumbani mwao.
Kwa wavulana, hatari hiyo iliongezeka kwa asilimia 20%.
Mtafiti Dr Anja Heilmann, alisema: "utafiti wetu unaonyesha kuwa kwamba kuna ushahidi wa wazi wa uhusiano baina ya kuwana TV chumbani kwa mtoto na kuongezeka kwa uzito wa mwili kwa mtoto miaka michache baadae."
Watafiti wanasema hawawezi kuwa na uhakika juu ya nini kinachosababisha uhusiano baina ya kutazama TV na kuongezeka kwa mwili, lakini wanasema huenda sababu ikawa ni watoto wenye TV vyumbani kusinzia kwa muda mfupi wakitumia muda mrefu kuitazama katika vyumba vyao vya kulala ama ulaji wa kiholela wanapotazama TV.
Watafiti wanatoa wito wa kuandaliwa kwa mikakati ya uzuwia unene wa kupindukia miongoni mwa watoto kwa kuangalia njia za kukabliana na tatizo hili.
Katika waraka wao kwenye jarida, wanasema : "wakati screen za TV zikiendelea utengenezwa kuwa vyembamba zaidi, watoto wetu wanakuwa na unene zaidi ."
tabia ya Ulaji usiofaa
Na kuna baadhi ya matokeo ya uchunguzi yaliyobaini kuwepo kwa uhusiano baina ya muda wasichana wanaoketi mbele ya TV na kuongezeka kwa uzito wa mwili husababishw ana kwamba wasichana hufanya mazoezi ya mwili kidogo kuliko wavulana wenye umri sawa na wao.
Profesa Russell Viner, kutoka chuo cha tiba na afya ya watoto cha Royal College (RCPCH) anasema matokeo ya utafiti huo yanapaswa kuchukuliwa kwa umakini zaidi.
Prof Viner anasema utafiti huo unaunga mkono haja ya kuzuwia ulaji wa vyakula visivyo na virutubisho vya mwili pamoja na matangazo ya TV yanayonadi vyakula hivyo
0 comments:
Post a Comment