Friday 2 June 2017

Taarifa mpya ya kinachoendelea kuhusu mwili wa Mzee 'Ngosha' aliyechora nembo ya taifa

Mwili wa Mzee Francis Maige Kanyasu alimaarufu kwa jina la Mzee Ngosha ambaye anayetajwa kuwa ni moja wa wachoraji wa nembo ya Taifa aliyefariki tarehe 30 mwezi wa 5 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili. unatarajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Misungwi Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Maendeleo ya Jamii) imesema kuwa ndugu wa Mzee Kanyasu wamepatikana na sasa serikali itagharamia kusafirisha mwili wa mzee huyo mpaka Mwanza ambapo atakwenda kuzikwa huko. 

Mwili wa Mzee Francis Maige unatarajiwa kuagwa kesho Jumamosi saa 2 asubuhi Hospitali Taifa ya Muhimbili kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza. 

0 comments:

Post a Comment