Friday, 2 June 2017

Obama anunua nyumba ya $8.1m ya kuishi Washington DC

Mali ya Obama ikihamishiwa Washinton baada yake kuondoka White House mwezi JanuariHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMali ya Obama ikihamishiwa Washinton baada yake kuondoka White House mwezi Januari
Familia ya Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama imenunua nyumba ambayo kwa muda wamekuwa wakiishi kwa kukodisha mjini Washington DC.
Nyumba hiyo yenye vyumba tisa inapatikana katika mtaa wa kifahari wa Kalorama na iliuzwa $8.1m (£6.2m).
Obama ameamua kuendelea kukaa Washington na familia yake hadi binti yake mdogo, Sasha ambaye ana umri wa miaka 15, amalize masomo ya shule ya upili.
Kiongozi huyo na mkewe Michelle wamekuwa wakizuru mataifa mbalimbali duniani tangu walipoondoka White House mwezi Januari.
Msemaji wa Bw Obama, Kevin Lewis, alithibitisha ununuzi huo na kusema: "Ikizingatiwa kwamba Rais na Bi Obama watakuwa Washington kwa angalau miaka mingine miwili unusu, ina umuhimu kwao kununua nyumba badala ya kuendelea kukodi."
Kuna vizuizi vya saruji kuzuia watu kufikia nyumba hiyo yenye ukubwa wa futi mraba 8,300 (mita mraba 770), ambayo inalindwa saa 24 kila siku na maafisa wa kikosi cha kulinda marais Marekani.
Familia ya Obama bado inamiliki nyumba Chicago.
Walinunua nyumba hiyo kutoka kwa aliyekuwa afisa wa habari wa Bill Clinton Joe Lockhart, aliyeinunua mwaka 2014 kwa $5.3m.
Nyumba hiyo haiko mbali sana na nyumba ya thamani ya $23m inayomilikiwa na mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos, ambaye pia humiliki gazeti la Washington Post.
Bintiye Rais Donald Trump, Ivanka, na mumewe Jared Kushner ambaye kwa sasa ni mshauri mkuu White House, pia wanaishi hapo karibu.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ni afisa mwingine wa ngazi ya juu anayeishi Kalorama, katika nyumba aliyoinunua kwa $5.6m Februari.

Related Posts:

  • Neema Ajira zaidi za 250 Wizara ya Ardhi SERIKALI imezidi kutangaza neema ya ajira kwa Watanzania baada ya kubainisha kuwa katika mwaka ujao wa fedha watumishi wapya 291 wataajiriwa katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Waziri wa wizara hiyo… Read More
  • Dola ya Marekani inateteleka WATUNGA sera kutoka Benki Kuu ya Marekani, wamesema wanafuatilia kilichoko katika uchumi wa taifa, kutokana na kuongezeka kiwango cha riba za benki nchini humo na imefanya thamani ya fedha za dola kushuka.Mchumi wa nchi hiy… Read More
  • CCM yajitosa uhalifu Kibiti CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uhalifu unaoendelea kutokea wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani unatosha na kuitaka vyombo vya ulinzi na usalama kulichukulia suala hilo kwa uzito likome.Kimesema yeyote mwen… Read More
  • Hatimaye simu mpya za Nokia 3310 zaingia madukani  Simu hizo mpya za Nokia 3310 zitakaa muda mrefu na chaji kuliko simu asiliSimu za Nokia 3310 zimeanza kuuzwa tena madukani, takriban miaka 17 baada ya simu hizo kuanza kuuzwa mara ya kwanza.Simu za sasa zina kamera ya… Read More
  • Aua mkewe kisa pesa ya matibabu JESHI la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Pastory Chilangazi (37), mkazi wa Kijiji cha Mamvisi, Wilaya ya Gairo kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kipigo kutokana na kile kinachoelezwa ni kutofautiana baada ya mkewe huyo ku… Read More

0 comments:

Post a Comment