Wednesday, 26 July 2017

Serikali yatangaza ajira 3,152 sekta ya afya

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo imetangaza ajira 3,152 kwa ajili ya wahitimu wa kada mbalimbali za afya nchini.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na wizara hiyo, ajira hizo ambazo zinatolewa kwa kibali cha wizara ya utumishi na utawala bora, ni kwa ajili ya watumishi kutoka kada 33 za afya.

Baadhi ya kada zilizotangazwa ni pamoja na madaktari, wataalam wa maabara, wauguzi/wauguzi wasaidizi, matabibu wasaidizi, wataalam wa meno, wataalam wa afya ya mazingira, wataalam wa mionzi, wataalam wa takwimu za afya, makatibu muktasi katika sekta ya afya, wataalam wa usafi, washauri wa afya, wafamasia n.k

Ajira hizo zinawahusu wahitimu wote wenye sifa stahiki za kitaaluma na hazitawahusu wahitimu wenye umri zaidi ya miaka 45, wahitimu ambao tayari ni waajiriwa wa serikali au wa mashirika wanaolipwa na serikali, pia hazitawahusu watu wote ambao wamewahi kufanya kazi serikalini na kuacha.

Ujio wa ajira hizi, ni tulizo la nafsi kwa wahitimu ambao wamekuwa wakisubiri ajira serikalini kwa takriban miaka miwili tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya tano, ambayo mwaka jana ilisitisha ajira kwa ajili ya kupisha zoezi uhakiki wa watumishi hewa.

Pia ajira hizo ni kuanza kwa utekelezaji wa mipango ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 ambapo mara kadhaa imekuwa ikiahidi kutoa ajira zaidi ya 50,000.

Waombaji wote wametakiwa kutuma maombi yao kabla ya Agosti 11 mwaka.

Related Posts:

  • Dola ya Marekani inateteleka WATUNGA sera kutoka Benki Kuu ya Marekani, wamesema wanafuatilia kilichoko katika uchumi wa taifa, kutokana na kuongezeka kiwango cha riba za benki nchini humo na imefanya thamani ya fedha za dola kushuka.Mchumi wa nchi hiy… Read More
  • ACACIA WAPINGA UCHUNGUZI WA KAMATI VITA kubwa. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Rais Dk. John Magufuli kuanza kuchukua hatua kali dhidi ya usafirishaji wa mchanga unaodaiwa kuwa na dhahabu. Baada ya hatua hiyo ya Rais Magufuli, kumeanza kuibuka mambo kadh… Read More
  • LUKUVI ATANGAZA KITANZI KWA MADALALI WA ARDHI tarajia kuandaa sheria itakayowabana madalali katika sekta ya ardhi. Amesema lengo la sheria hiyo ni kuwabana madalali hao ambao wamekuwa wakiuza ardhi katika siku za mapumziko kutokana na sababu wanazozijua wao. Lukuv… Read More
  • TAMKO LA SERIKALI: WANAJESHI HAWANA HAKI YA KUTESA RAIA SERIKALI imesema hakuna sheria yoyote inayowapa haki wanajeshi kutesa raia au kuvunja sheria. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu… Read More
  • Hatimaye simu mpya za Nokia 3310 zaingia madukani  Simu hizo mpya za Nokia 3310 zitakaa muda mrefu na chaji kuliko simu asiliSimu za Nokia 3310 zimeanza kuuzwa tena madukani, takriban miaka 17 baada ya simu hizo kuanza kuuzwa mara ya kwanza.Simu za sasa zina kamera ya… Read More

0 comments:

Post a Comment