Monday, 19 June 2017

Ole Sendeka atuma salamu hizi kwa Lowassa

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amempongeza Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kumpongeza Rais John Magufuli kufuatia uamuzi aliouchukua kuhusu mchanga wa madini yanayochimbwa nchini na kampuni ya Acacia.

Ole Sendeka ambaye aliwahi kuwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, amesema kuwa baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amempongeza Rais, hana budi kumshukuru na kumpongeza pia kwa kufanya hivyo, na kuwaomba wabunge wote bila kujali vyama vyao kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kusimamia kikamilifu rasilimali za nchi.

“Nanyi wabunge mkiwa bungeni muungeni mkono Rais wetu Magufuli anavyotetea rasilimali za nchi ili madini yanayochimbwa yaweze kuwanufaisha Watanzania, waweze kupata huduma zao za msingi kupitia madini hayo,” Ole Sendeka anakaririwa na Mwananchi.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza jana kwenye mazishi ya mama yake mzazi yaliyofanyika katika kijiji cha Losokonoi wilayani Simanjiro.

 Alimuomba mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya ambaye alihudhuria mazishi hayo, kumfikishia salamu na pongezi hizo kwa Lowassa.

Lowassa alimpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake baada ya kupokea ripoti ya pili ya uchunguzi wa makontena ya mchanga wa madini yanayoshikiliwa na Serikali katika bandari ya Dar es Salaam, yalipokuwa katika mchakato wa kusafirishwa nje ya nchi na kampuni ya Acacia.

Simba yatumia Mil. 100/ kumshawishi Niyonzima

NI UMAFIA TU! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima kudaiwa kujiunga na Klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kupewa ofa ya Sh. milioni 100.

Habari zilizopatikana jana jioni zinasema Niyonzima amekubali kujiunga na Simba baada ya viongozi wa klabu hiyo kumpa fedha hizo za usajili.

Kwa muda mrefu tangu kumalizika kwa Ligi Kuu Bara, Niyonzima ambaye amebakisha mwezi mmoja kwenye mkataba wake na Yanga, alikuwa akihusishwa kutaka kujiunga na Simba.

Taarifa zinadai kuwa Simba waliongea na Niyonzima kabla hajaenda Rwanda kujiunga na timu yake ya Taifa, lakini akataka viongozi hao kuwasiliana na wakala wake ambapo Simba walifanya hivyo na kupewa dau walilokuwa wakilitaka.

Aidha, Yanga iliwasiliana na Niyonzima akiwa Rwanda baada ya kusikia Simba wamewasiliana naye na hivyo wakamuahidi ofa nono ili asisajiliwe na Simba.

Baada ya kusikia Yanga wamewasiliana na Niyonzima, Simba walimtuma mtu kwenda Rwanda kufanya mazungumzo na mchezaji huyo, lakini wakala wake aliwataka wamsubiri Niyonzima Dar es Salaam kwa kuwa alikuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

Niyonzima alipowasili nchini juzi usiku alipokelewa na kigogo mmoja wa Simba huku Yanga wakiwa hawafahamu kama nyota huyo ametua nchini.

Imeelezwa Yanga walimuandalia nyota huyo dau la Sh. milioni 60 ili asaini mkataba wa miaka miwili, lakini tajiri mmoja wa Simba alimuhakikishia kumpa dau la Sh. milioni 100.

Kabla ya kupewa dau hilo, Yanga waliongezea dau lao na kufikia Sh. milioni 80 ambazo hata hivyo, hazikumshawishi nahodha huyo wa Rwanda kusaini nao mkataba mpya.

Aidha, pia Simba juzi ilimalizana na kiungo na nahodha wake, Jonas Mkude kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili.

Mkude pia alikuwa akiwindwa na Yanga iliyoibomoa Simba kwa kumsajili mshambuliaji wao, Ibrahimu Ajib.

Nchemba amtolea uvivu Tundu Lissu

 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ‘amemvaa’ Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kwamba amejaribu kutengeneza kila aina ya kichaka kukwamisha jitihada za Rais John Magufuli kupambana na usafirishaji holela wa madini nje ya nchi bila mafanikio.

Ingawa Mwigulu hakumtaja jina Lissu moja kwa moja alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Zinzirigi kilichopo katika Jimbo lake la Iramba Magharibi pia mkoani Singida juzi, hoja nyingi alizogusia ni zile ambazo Lissu amekuwa akinukuliwa kuzisema.

Moja ya hoja hizo ni ile ambayo Mwigulu alisema watu wenye nia mbaya walianza kusema kuwa Serikali itashtakiwa kwa hatua yake ya kuzuia makontena 277 ya mchanga wenye dhahabu.

“Baadaye watu haohao walisema tena kwamba mchanga ule ni takataka tu lakini walipoambiwa wasisafirishe mchanga huo wenye madini walisema wanapata hasara ya Sh4 trilioni kwa siku.”

Hata hivyo, Acacia walisema wanapata hasara ya dola bilioni moja kila siku.

Pia, Mwigulu alisema tangu Rais Magufuli alipounda kamati mbili kufuatilia suala la mchanga huo wa madini, watu hao aliowaita kuwa ni wenye nia mbaya walianza kutumia majina ya marais wastaafu Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa kama kichaka ili Serikali iache kufuatilia sakata hilo la mchanga wa madini.

“Hawa watu walikuwa wanatuona kama mazuzu hivi. Rais wetu amechukua hatua tena siyo kwa maneno, kwa vitendo. Tumuunge mkono,” alisema Mwigulu.

Tangu kuanza kwa sakata hilo la mchanga wa madini, Lissu amekaririwa mara kwa mara akisema kwamba suala hilo linashughulikiwa kisiasa badala ya kisheria jambo linaloiweka Tanzania katika hatari ya kushtakiwa na kushindwa.

Pia alikaririwa bungeni akisema Rais Kikwete anaponaje katika sakata hilo na jana alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Nchemba alisema msimamo wake uko palepale kuhusu sakata hilo.

Alichosema Mwigulu

Mwigulu aliwaeleza wananchi hao kwamba viongozi wa Tanzania hawajawahi kuwa mawakala wa wale wanaoliibia Taifa na kwamba Watanzania wamewaona mawakala wa wezi hao kwa sababu wanawatetea. “Na mimi nimpongeze Rais kwa kuuona ule mtego, akafyatua pyaa! Sasa hivi kama ni gari lao matairi yote, Rais kashayaondoa upepo, yameshalala chini. Maana lile walitaka kutengeneza mtego, yaani ni kama mtu anayepigwa anatafuta mti ili ajifiche,” alisema Mwigulu.

Alisema heshima ya nchi hii kwa viongozi wastaafu waliofanya kazi nzuri ndiyo inayowafanya viongozi wa Taifa hili wasing’ang’anie madarakani, jambo ambalo mataifa mengine wameshindwa kufanya.

“Kama leo una uhakika ukiondoka madarakani unashtakiwa, kwa nini uondoke madarakani?” alihoji Mwigulu na kusisitiza kwamba alichofanya Rais Magufuli ni kulinda heshima za viongozi wastaafu.

Aliwataka wananchi kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kulinda rasilimali za Taifa kwa sababu ndiyo zinazowawezesha kuwapatia maji, barabara za lami, umeme, elimu bure na dawa.

Lissu ajibu

Akizungumzia kauli ya Mwigulu kwamba wanajificha kwenye kichaka cha viongozi wastaafu ili kufifisha jitihada za Rais Magufuli, Lissu alisema ni ukweli ulio wazi kwamba huwezi kuwataja wahusika wa mikataba mibovu ya madini bila kurudi nyuma.

“Tunawaacha kwa sababu hatuwawezi. Kwa sababu wana kinga,” alisema Lissu na kusisitiza kwamba wanataka kuona wanapata chanzo halisi cha uzembe uliofanyika na siyo kuonea watendaji wadogo.

Lissu alisema Sheria za Madini na mikataba mingi ilisainiwa miaka ya 1997 na 1998.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alieleza kushangazwa na Serikali kuacha kuzungumzia kwamba kampuni ya Acacia haijasajiliwa badala yake Rais Magufuli amekubali kukaa na wale anaowaita wezi ili kujadiliana.

Hatua zilizochukuliwa

Tangu sakata la mchanga wa madini lilipoanza, Rais Magufuli amechukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kutengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na ofisa mtendaji mkuu wake na kuagiza viongozi na watendaji wengine kuchunguzwa na vyombo vya dola.

Ripoti ya kamati ya pili iliyoongozwa Profesa Nehemiah Osoro imewataja baadhi ya viongozi waliohusika katika kuingia mikataba tata na kupendekeza Serikali iwachukulie hatua.

Waliotajwa kwenye taarifa ya kamati ya pili iliyowasilishwa kwa Rais Magufuli Juni 12 ni waliokuwa mawaziri katika Wizara ya Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, William Ngeleja, Nazir Karamagi, Daniel Yona na Dk Abdallah Kigoda ambaye kwa sasa ni marehemu.

Wengine ni waliokuwa wanasheria wakuu, Andrew Chenge na Johnson Mwanyika; manaibu wanasheria wakuu Felix Mrema na Sazi Salula; makamishna wa madini, Paulo Masanja, Dk Dalaly Kafumu na Ally Samaje na wakuu wa idara ya mikataba, Maria Ndosi Kejo na Julius Malaba.

Akizungumzia kutajwa kwake katika ripoti ya kamati ya pili, Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja alisema bungeni kwamba “kutuhumiwa siyo kukutwa na hatia, maisha yanaendelea.”

Viongozi wengine waliotajwa katika ripoti hiyo hawajajitokeza kuzungumzia suala hilo.
source:muungwana

Hoja 6 moto mkali kwa serikali bungeni

MJADALA wa mapendekezo ya makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 unatarajiwa kuhitimishwa leo mjini hapa huku hoja sita zikionekana kuwa mtihani mgumu kwa serikali kuzitolea majibu kesho wakati inahitimisha mjadala huo kabla ya wabunge kupiga kura ya wazi ya kuipitisha kesho 

Kwa mujibu wa ratiba ya mkutano wa Bunge la Bajeti, baada ya mjadala wa bajeti ya serikali kuhitimishwa leo na wabunge kupitisha bajeti kwa kura ya wazi kesho, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango, atawasilisha Muswada wa Sheria ya Fedha za Matumizi.

Kwa siku ya nane mfululizo wabunge wamekuwa wakijadili mapendekezo ya makadirio ya bajeti hiyo ya Sh. trilioni 31.7 huku mjadala huo ukionekana 'kutekwa' na sakata la makinikia.

HOJA SITA MOTOUtunishaji wa mfuko wa maji, mfuko wa mazingira, ujenzi wa reli ya kisasa Dar es Salaam -Tanga-Musoma  na ujenzi wa zahati kila kijiji na kituo cha afya kila kata ni miongoni mwa hoja sita ambazo zinatarajiwa kuwa mtihani mgumu kwa serikali wakati wa kuhitimisha mjadala huo kesho.

Nyingine ni uimarishaji wa Kampuni ya Simu (TTCL) na kufutwa kwa ada ya mwaka ya leseni za magari yaani 'road licence fee'.  

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Hawa Ghasia, aliliambia Bunge Jumatatu iliyopita kuwa kamati yake ilipokea hoja zilizojitokeza wakati wa kujadili na utekelezaji wa bajeti za wizara mbalimbali kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 na makadirio ya bajeti zake kwa mwaka ujao wa fedha.

Alisema katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuliibuka hoja ya TTCL iongezewe mtaji ili iweze kuchangia pato la taifa.

Alisema kamati yake ilikubaliana na hoja hiyo na kupendekeza kwa kuanzia kampuni hiyo ipewe Sh. bilioni 295.2 kama mtaji, lakini majibu ya serikali hayaonyeshi ni kiasi gani itaipatia TTCL.

Ghasia alisema hoja ya pili ilihusu kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam-Musoma kupitia Tanga, Moshi na Arusha na kwamba kamati ilipendekeza fedha za mfuko wa reli zitumike kulipia gharama za upembuzi yakinifu na upembuzi wa kina.

Hoja ya tatu ilitoka Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo inataka Mfuko wa Mazingira uwezeshwa kifedha na ilipendekeza ikatwe asilimia tano kutoka kwenye vyanzo 11 vinavyohusu tozo mbalimbali za wizara na taasisi ili mfuko huo upate fedha za kujiendesha.

Ghasia alisema kuwa katika majibu yake mbele ya kamati hiyo, serikali haikuonyesha kuwa kiasi cha Sh. bilioni 13 kinaweza kupatiana kutoka vyanzo husika.

Hoja ya nne ni kuongeza bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kuongeza tozo ya Sh. 50 kwa kila lita ya petroli na dizeli kwa ajili ya kutunisha Mfuko wa Maji.

Ghasia alisema kamati yake inapendekeza asilimia 70 ya makusanyo itumike kwa ajili ya kuboresha maji vijijini na asilimia 30 ya makusanyo itumike kwa ajili ya maji maeneo ya mijini.

Alisema hoja ya tano ilitoka kwenye Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambapo kamati yake ilitaka kujua gharama halisi za ujenzi wa kila kituo cha afya na zahanati pamoja na kiasi cha fedha ambacho kimetengwa na serikali na kutekeleza ujenzi huo katika mwaka ujao wa fedha.

Alisema majibu ya serikali ni kuwa imetenga Sh. bilioni 69 kwa ajili ya kuanza na kukamilisha ujenzi wa maboma ya zahanati 1,538 na vituo vya afya 244 na kwamba baada ya mashauriano na serikali, kamati yake ilikubali majibu hayo.

Hoja hiyo ililazimika kufikishwa mbele ya kamati hiyo baada ya wabunge wote kuungana kuitaka serikali itekeleze ahadi yake ya kujenga zahanati kila kijiji na kituo cha afya kila kata ili kupunguza vifo vya uzazi ambavyo kwa sasa ni 556 katika kila vizazi hai 100,000 nchini.

Kuhusu kufutwa kwa ada ya mwaka ya leseni za magari yaani, Ghasia alisema imeondoa kero kubwa kwa wananchi hivyo kurudisha imani kwa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Alisema hatua hiyo pia itaongeza mapato ya serikali kuliko ilivyokuwa awali na kwamba kamati inashauri kutumia kiasi cha Sh. 40 kitakachoongezwa kwenye mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kipelekwe kwenye mfuko wa maji kwa ajili ya miradi ya maji vijijini.

Mbali na hoja hizo zilizofikishwa mbele ya kamati ya Ghasia, wabunge wa upinzani wakati wa mjadala wamekuwa wakilalamikia kitendo cha serikali kuu kuchukua baadhi ya kodi za serikali za mitaa zikiwamo za majengo, ardhi na mabango ya matangazo.

Ally Mayay, Mtemi kuwania urais TFF

 MAYAY

Ally Mayay anatarajia kuchukua nafasi ya kuwania Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Taarifa zinaeleza Mayay ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, atachukua fomu hizo leo.

MTEMI

Wakati Mayay anachukua fomu, mshambulizi matata wa zamani wa Simba, Mtemi Ramadhani “Mangi” naye anatarajia kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Makamu Rais wa TFF.

Imeelezwa, wachezaji hao watasindikizwa na wanasoka wa zamani wa klabu mbalimbali za soka.

Zitto aukataa Urais TFF

Ijumaa ya Aprili 21, mwaka huu, gazeti la michezo na burudani nchini, Mwanaspoti, liliandika habari kwenye ukurasa wake wa kwanza yenye kichwa: "Zitto ajitosa Urais TFF, Rage amkubali."

Upande wangu, licha ya kwamba habari hiyo ilichapishwa bila kupata maoni yangu, lakini haikuwa ngeni. Hii ni kwa sababu kabla ya habari hiyo nilikuwa nimeshapokea maombi kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwemo viongozi wakubwa wakinitaka nigombee Urais TFF.

Baada ya habari hiyo kuchapishwa na kupata umaarufu mkubwa, nilipokea maombi mengi zaidi pamoja na shinikizo lenye kunitaka muda ukifika wa uchukuaji fomu, nijitokeze nichukue fomu ya kuwania Urais TFF.

Msukumo ni mkubwa na maswali ni mengi kipindi hiki ambacho dirisha la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi TFF limefunguliwa.

Kila ombi na shinikizo ambalo nimepokea, nimelibeba kwa unyenyekevu mkubwa. Bila shaka wanaoniomba na kunishinikiza wanavutwa na mambo mawili; mosi, soka letu kutoleta nuru kwa Watanzania. Pili, imani kubwa kwamba kupitia uongozi wangu nuru ya soka letu itadhihirika.

Hata hivyo, yapo mambo mawili nimeyatafakari; Mosi, mahitaji ya soka letu na nguvu ya maarifa inayohitajika kulikwamua. Pili, nafasi yangu kama mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Kuhakikisha kazi ya kulikwamua soka letu inafanikiwa na nuru inadhihirika kwa wapenda soka wote nchini, inahitaji uwekezaji mkubwa wa muda, vilevile uwekezaji mkubwa wa maarifa ya kiuongozi.
Soka la Tanzania lipo hapa kwa sababu ya uwekezaji usioridhisha wa maarifa ya uongozi, hiyo inatokana pia na viongozi wanaopata nafasi ya kulitumikia shirikisho letu la mpira wa miguu nchini, kutowekeza muda wao barabara kwenye soka.

Nikiwa Kiongozi wa ACT-Wazalendo, ninadaiwa mambo mawili, uwekezaji wa muda na uwekezaji wa maarifa ya kiuongozi ili kukiandaa vema chama chetu kushiriki uchaguzi kati ya miezi 28 mpaka 40 inayokuja.

Mwaka 2019, Chama kitashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mwaka 2020, Chama chetu kitashiriki Uchaguzi Mkuu.

Hivyo basi, kwa kuongezea na uwakilishi wangu wa Jimbo la Kigoma Mjini ambako Chama chetu kinaongoza Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, naona kuwa lipo eneo ambalo nitashindwa kulitimizia wajibu wake nikivaa kofia ya tatu ya Urais wa TFF.

Nimetafakari na kuchukua uamuzi kwamba Uongozi wa ACT-Wazalendo na Ubunge ni nafasi ambazo ninazo tayari, wakati Urais TFF ni nafasi mpya.

Kwa hali hiyo na kwa mapenzi makubwa ya soka la Tanzania, nimeamua nisichukue fomu ya kugombea Urais wa TFF, kwani naweza kuomba kazi ambayo nitashindwa kuitumikia kwa muda wa kutosha kutokana na majukumu yangu kwenye Chama na ubunge.

Uamuzi huu umezingatia mapenzi makubwa kwa soka letu. Nikijitokeza kuwania Urais wa TFF leo halafu nikakosa muda mzuri wa kutimiza matarajio ya wapenda soka nchini, utakuwa usaliti mkubwa kwa maendeleo ya soka la Tanzania.

Nawashukuru wote walioniomba na kunishinikiza nichukue fomu. Nawaambia kuwa kwa sasa tujielekeze kupata viongozi bora miongoni mwa watakaojitokeza. Wakati mwingine mazingira yakiruhusu, nitaweza kutii maombi hayo.
Asante sana.

Zitto Zuberi Kabwe Ruyagwa

Saturday, 17 June 2017

Wezi wavamia Nyumba, Wachinja kuku, wakapika, kula na kuosha vyombo


Charity Njeri akionesha Masufuria yaliyutumika kupikia kuku

Wezi wamevamia nyumba moja huko Kenya na kuchinja kuku, kupika, kula & kuosha vyombo kabla ya kutokomea na mali zenye thamani isiyojulikana.

Kwamujibu wa Mtandao wa Standard Digital wa nchini Kenya Umeripoti hivi...

"Thugs broke into a pastor’s house in Mweiga, slaughtered and cooked his chicken then washed dishes.

Pastor Joseph Muraya said the thieves got into his compound around 8pm and threatened to shoot them if they alerted neighbours.

“I came back at around 8pm and was surprised to see the gate half open. I heard the dogs bark and when I went out to check, I saw someone outside. I later realised there were five more inside,” he said.

They made away with property of unknown value. Deputy County Police Commander Peter Okiring’ said the police have launched investigations."

Kaburi la baba wa Spika wa Bunge Job Ndugai lafukuliwa

Wananchi wanafukua mabaki ya mwili wa baba wa Spika wa Bunge Job Ndugai, Yustino Ndugai aliyezikwa Bukombe ili kuyapeleka Kongwa.

source:mwananchi

Umuhimu wa kufanya mazoezi ya kutembea

Mazoezi ni muhimu kwa kila mmoja wetu, kwa sababu hayana uitaji wa gharama kubwa ukilinganisha na aina nyingine za mazoezi.

Pia kutembea kwa kasi kwa muda wa saa moja na kuendelea imesadikika ya kwamba kuna faida zifuatazo;

1. Husaidia kuimarisha mifupa.

2. Husaidia kwa kiwango kikubwa katika kupunguza mfadhaiko/ stress.

3. Humfanya mtu ajisikie vizuri kiafya.

4. Hupunguza na kitibu shinikizo la damu.

5. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na matatizo yatokonayo na kolesto.

6. Mazoezi  hayo husaidia kupunguza uzito kwa kiwango kikubwa

7. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na magonjwa ya shambulio la moyo.

Fanya hivi pale mtoto mchanga anapopatwa na kwikwi.

Kwikwi ni kitu cha kawaida kutokea hasa umri unavyozidi kwenda. Na mtoto mchanga yupo kwenye hatari zaidi ya kupata kwikwi, pia hata ndani ya mfuko wa kizazi kuanzia wiki ya sita mtoto huweza kupata kwikwi. Kwikwi hizi huweza kuwepo kati ya dakika moja hadi saa bila kuleta madhara yoyote kwa mtoto.

Chanzo cha kutokea kwa kwikwi kwa mtoto.
Kwikwi husababishwa na kusinyaa kwa misuli kitaalamu diaphragm(contraction or irritation of diaphragm) ambayo hutenganisha kifua na tumbo, na kwa madaktari bingwa wa watoto wanasema pia kwikwi huweza kusababishwa na aina ya vyakula, vyakula hivyo ni kama (maziwa anayonyonya kutoka kwa mama, au maziwa ya kopo) mara nyingine inaelezwa ya kwamba kutokea kwa kwikwi kwa mtoto husababishwa na na joto la mtoto linaposhuka sana.

Kwikwi huwa hatari sana pale inapotekea mara kwa mara na kutopata nafuu, na kusababisha mtoto kushindwa kunyonya, kula na kulala. Hivyo inapotekea hali hii mpe mtoto maji kidogo, huku ukimsugua mgongo. Unaweza kutumia Grip water. Mpe mtoto chakula akiwa ametulia, na jaribu kubadilisha mkao wa mtoto, na kumtuliza mtoto na hali hii inaweza kuisha.
 mpe mtoto Grip water kwa kipimimo cha 0.5mm

Ukiona hali hii haiiishi ni vyema kwenda kwa daktari bingwa wa watoto mapema iwezekanavyo, ili uweze kupata msaada wa kitaalamu.