Monday, 15 May 2017

Mahabusu aomba adhabu ya kifo cha kumiminiwa risasi Marekani

JW Leford amekuwa akitumia dawa ya kupunguza maumivu ya nevi ambazo mawakili wake wanasema huenda zikabadili utendakazi wa ubongo wake
Mahabusu anayesubiri kunyongwa katika jela moja katika jimbo la Georgia nchini Marekani amewasilisha ombi la kuuawa kwa kuumiminiwa risasi kwa sababu kifo cha kuuawa kwa kudungwa sindano kina uchungu mno.
JW Leford amekuwa akitumia dawa ya kupunguza maumivu ya nevi ambazo mawakili wake wanasema huenda zikabadili utendakazi wa ubongo wake na kumfanya kuwa na uchungu mkali kinyume na katiba.
Ledford alihukumiwa 1992 kwa kumuua jirani yake.
Jaji mmoja alikataa ombi lake siku ya Ijumaa lakini mawakii wake wamesema kuwa watakata rufaa .
Anatarajiwa kunyongwa siku ya Jumanne.
Mawakili wake wamesema kuwa katika nakala za mahakamani kwamba Leford amekuwa akitumia dawa ya gabapentin kwa zaidi ya muongo mmoja.
Wametaja wataalam ambao wanasema kuwa utumizi wa muda mrefu wa gabapentin unaathiri ubongo kwa hali ya kwamba dawa ya Pentobarbital itakayotumika katika kumdunga sindano wakati wa kuuawa kwake haiwezi kuuwa tegemo kumfanya kukosa fahamu na kupoteza hisia .


SOURCE:BBC

0 comments:

Post a Comment