Rais Magufuli ameridhia maombi ya watatu hao kutaka kuacha kazi
Majaji wawili wa Mahakama Kuu nchini Tanzania wameacha kazi, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Taarifa hiyo inasema majaji Aloysius Kibuuka Mujulizi na Upendo Hillary Msuya wamewasilisha maombi ya kuacha kazi kwa rais, ambayo yamekubaliwa.
Jaji Mujulizi alikuwa pia mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria Tanzania.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadiki pia ameacha kazi.
Taarifa ya ikulu haijaeleza sababu iliyowafanya maafisa hao watatu kuamua kuomba kuacha kazi.
source:bbc
0 comments:
Post a Comment