Tuesday, 23 May 2017

Nyumba zateketea kwa moto Sengerema


Sengerema. Nyumba za wavuvi ambazo idadi yake haijajulikana hadi sasa katika kisiwa cha uvuvi cha Nyamango Kata ya Bulyaheke  halmashauri ya Buchosa wilayani hapa, zinateketea kwa moto ambapo chanzo chake hakijajulikana.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole umesema moto huo umezuka ulianza saa 8.00 mchana na juhudi za kuuzima zinaendelea kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama.

Kwa mjibu wa mkuu wa wilaya zaidi ya uharibifu wa mali hakuna taarifa ya mtu kupoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo ambalo ni mwendelezo wa matukio kadhaa ya mioto katika visiwa vya uvuvi wilayani humo.

Diwani wa Kata ya Bulyaheke, Bageti Ngele amesema juhudi za wananchi za kudhibiti moto huo hazijazaa matunda kutokana na nyumba hizo kujengwa kwa mbao na mabanzi.

Related Posts:

  • Aua mkewe kisa pesa ya matibabu JESHI la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Pastory Chilangazi (37), mkazi wa Kijiji cha Mamvisi, Wilaya ya Gairo kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kipigo kutokana na kile kinachoelezwa ni kutofautiana baada ya mkewe huyo ku… Read More
  • Dola ya Marekani inateteleka WATUNGA sera kutoka Benki Kuu ya Marekani, wamesema wanafuatilia kilichoko katika uchumi wa taifa, kutokana na kuongezeka kiwango cha riba za benki nchini humo na imefanya thamani ya fedha za dola kushuka.Mchumi wa nchi hiy… Read More
  • Neema Ajira zaidi za 250 Wizara ya Ardhi SERIKALI imezidi kutangaza neema ya ajira kwa Watanzania baada ya kubainisha kuwa katika mwaka ujao wa fedha watumishi wapya 291 wataajiriwa katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Waziri wa wizara hiyo… Read More
  • CCM yajitosa uhalifu Kibiti CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uhalifu unaoendelea kutokea wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani unatosha na kuitaka vyombo vya ulinzi na usalama kulichukulia suala hilo kwa uzito likome.Kimesema yeyote mwen… Read More
  • Hatimaye simu mpya za Nokia 3310 zaingia madukani  Simu hizo mpya za Nokia 3310 zitakaa muda mrefu na chaji kuliko simu asiliSimu za Nokia 3310 zimeanza kuuzwa tena madukani, takriban miaka 17 baada ya simu hizo kuanza kuuzwa mara ya kwanza.Simu za sasa zina kamera ya… Read More

0 comments:

Post a Comment