Monday, 22 May 2017

Rubani aliyeiba ndege ya Usovieti na kuipeleka Japan

Ndege ya XB-70 bomber ina uwezo wa kasi mara tatu kuliko sauti
Tarehe 6 mwezi Septemba mwaka 1976 ndege ilionekana ghafla kutoka kwenye mawingu karibu na mji wa Hakodate katika kisiwa kilicho kaskazini cha Hokkaido nchini Japan
Ilikuwa ndege yenye injini mbili lakini haikuwa ndege ya kawaida ambayo watu wa Hakodate walikuwa wamezoea kuiona.
Ndege hiyo kubwa iliyokuwa na alama za Muungano wa Usovieti haikuwa imeikana eneo hilo.
Ilitua katika uwanja wa Hakodate. Barabara ya uwanja wa ndege ilikuwa fupi hali iliyolazimu ndege hiyo kuchimbua ardhi ilipomaliza kukimbia kwenye barabara na kusimama mwisho kabisa mwa uwanja wa ndege.
Rubani akachomoza kutoka chumba cha rubani na kufyatua risasi mara mbili hewani kutoka kwa bastola yake.
Dakika kidogo baadaye maafisa wa uwanja wa ndege wakamkaribia. Huu ndio wakati rubami mwenye umri wa miaka 29 Luteni Viktor Ivanovich Belenko wa jeshi la wanahewa wa Usovieti alitangaza kuwa alitaka kuhama.
Ndege hiyo aina ya Mikoyan-Gurevich MiG-25 ndiyo ndege yenye usiri zaid kuwai kuundwa na muungano wa usoviet.
Marekani ilidhani kuwa ndege hiyo ilikuwa na uwezo mkubwaHaki miliki ya pichaUS NAVY
Image captionMarekani ilidhani kuwa ndege hiyo ilikuwa na uwezo mkubwa
Nchi za magharibi ziligundua kitu ambacho kilionekana kama ndege ya MiG-25 miaka ya sabini. Satelaiti za ujasusi zilikuwa zikichunguza viwanja vya usovieti zilichukua picha za ndege zilizokwa zikifanyiwa majaribio ya kisiri.
Zilionekana kama ndege kubwa za kivita na wanajeshi wa nchi za magharibi walikuwa na wasi wasi baada ya kuona kitu fulani: mbawa kubwa.
Mwezi Novemba mwaka 1971 Israeli ilikumbana na moja ya ndege hizo ikirusha makomba kutoka umbali wa futi 30,000 angani. Ndege hiyo ilikuwa na kasi ya mara tatu zaidi ya sauti . Ilikuwa ndege yenye kasi kubwa na tayari ilkuwa imeondoka eneo hatari kabla ya makombora ya Israel kupapa.
Jeshi la Marekani liliamini kuwa ndege hiyo ilikuwa ile ilionekana kupitia picha za Satelaiti. Ghafla waliamini kuwepo ndege ambayo ina uwezo kushinda ndege yoyote katika jeshi la Marekani.
Ndege ya MiG-25Haki miliki ya pichaUS NAVY
Image captionNdege ya MiG-25
Viktor Belenko, alikuwa raia wa Usovieti. Alizaliwa mara baada ya vita vya pili vya dunia eneo la milima ya Caucasus. Alijiunga na jeshi na kufuzu kama rubani wa ndege za kivita cheo ambacho kilikuwa na hadhi ya juu kuliko cha mwananchi wa kawaida.
Akiwa baba wa mtoto mmoja wakati huo, na akikabiliwa na talaka, pia alikuwa na maswali mengi kuhusu jamii ya usovieti
Belenko alifahamu kuwa ndege kubwa ya kijeshi ambayo aliitumia kujifunza ingekuwa njia muhimu ya kukimbia.
Akiwa katika kambi ya jeshi la hewa ya Chuguyevka karibu na mji wa mashariki wa Vladivostok. Japan ilikuwa umbali wa kilomita 644. Lakini ikiwa na injini kubwa inamaana kuwa haingeruka mbali sana hadi kutua katika kambi ya Marekani.
Kitambulisho cha Belenkokikos kwmney makavzi mjini WashingtonHaki miliki ya pichaCIA MUSEUM
Image captionKitambulisho cha Belenko kiko kwenye makavazi mjini Washington
Tarehe 6 mwezi Septemba Belenko aliondoka na marubani wenzane kufanya mazoezi. Mara moja akatafuta njia ya kupita kwa sababu ndege yake ilikuwa na mafuta ya kutosha. Alijiondoa na dakika chache baadaye alikuwa safarini kuelekea Japan.
Ili kukwepa mitambo ya rada ya Usovieti na ile ya Japan, Belenko aliruka chini kwa chini karibu futi 100. Lakini alipoingia anga ya Japan alipanda hadi futi 20,000 ili aweze kuonekana kwa rada za Japan. Wakati ndege za Japan ziliwekwa tayari Belenko alitoweka na kuingia ndani ya mawingu na kutoweka kutoka kwa rada za Japan
Belenko alikuwa na nia ya kuruka hadi uwanja wa Chitose lakinin ndege yake ilikuwa imeishiwa na mafuta kwa hivyo alitua uwanja uliokuwa karibu wa Hakdodate.
MiG-25 ilichangia kuundwa kwa ndege ya F-15, inayotumiwa Marekani hadi leoHaki miliki ya pichaISTOCK
Image captionMiG-25 ilichangia kuundwa kwa ndege ya F-15, inayotumiwa Marekani hadi leo
Ghafla Japana wakajikuta wakiwa na rubani aliyehama na ndege ya kivita ambayo imekuwa ikikwepa mashirika ya ujasusi ya nchi za magharibi.
Uwanja wa Hakodate ukakuwa wenye shughuli nyingi za ujasusi jambo ambalo hata CIA haikuamini.
Belenko hakurudi USSR wala ndege yake hiyo. Aliruhusiwa kuhamia nchini Marekani baada ya kupewa uraia na Rais Jimmy Carter ambapo alipewa cheo cha mhandisi wa ndege mshauri wa jeshi la Marekani. Kitambulisho na yale yote aliyoandika wakati akiwa safarini kuelekea Japan yako kwenye maonyesho kwenye makavazi ya CIA mjini Washingtona DC.


source:bbc

0 comments:

Post a Comment