Saturday, 13 May 2017

AJUCO THIRD YEAR WATUNISHIWA MISULI NA RMA


Katika kile ambacho hakikutarajiwa na mashabiki wengi wa AJUCO third year lakini kimewezekana ni baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya timu ya chuo cha wauguzi Songea maarufu kama RMA. Mechi hiyo ilichezwa katika uwaja wa RMA majira ya saa kumi na moja kasoro amabapo mshmbuliaji wa timu ya RMA Nickson aliweza kuipatia timu yake bao la kwanza mnamo dakika ya 7 na baadae mshambuliaji Luckuman kutoka RMA aliweza kuifungia timu yake hiyo goli la 2 mnamo dakika ya 29. Baada ya kipindi cha pili AJUCO third year waliweza kujipatia bao la kufutia machozi amabalo lilifungwa na msambuliaji Matambi mnamo dakika ya 85. Mechi hiyo ilimalizika huku AJUCO third year wakiambulia kipigo cha goli 2-1 dhidi ya  RMA.

Michuano hiyo ya ligi ya AJUCO itaendelea kesho majira ya saa nane mchana katika uwanja wa RMA amabapo AJUCO third year watacheza tena na AJUCO diploma , na baadae saa kumi jioni kutakuwa na mechi kati ya AJUCO second year na AJUCO First year 'B'.

Sonsoge blog itaendelea kukuletea habari zote za michuano ya ligi ya AJUCO, Tafadhali subscribe hapo juu ili uwe wa kwanza kupata taarifa.

0 comments:

Post a Comment