Sunday 14 May 2017

MWAKA WA TATU WAKUBALI KIPIGO TENA

Ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya AJUCO ligi (inter class), leo hii majira ya jioni hali imekuwa mbaya kwa wakongwe wa chuo cha AJUCO (third year) baada ya kukubali kipigo cha magoli 3-2 kutoka kwa wadogo zao mwaka wa kwanza 'B' katika mechi za ligi inayoendelea chuoni hapo. Magoli matatu yote ya timu ya Mwaka wa kwanza 'B' yalifungwa na kiungo wao mshambuliaji mahili BARAKA ambae pia hucheza namba 9 katika timu ya chuoni hapo. Pia magoli ya mwaka wa tatu yamefungwa na MATAMBI akifuatiwa na striker wa kutegemewa kwa mwaka wa tatu MUSTI (MUSTAPHA MOHAMED).



Vikosi vya mwaka wa tatu na wa kwanza

Hata hivyo Mwaka wa tatu wameshikwa na hali ya sintofahamu baada ya kukubali kipigo hicho cha magoli 3-2 kutoka kwa wadogo zao First year katika mechi iliyochezwa leo jioni katika viwanja vya RMA. Kipigo hicho kimepelekea mwaka wa tatu kutokuwa na matumaini ya kuendelea na  ligi hiyo.


mshambuliaji BARAKA aliyepiga HAT-TRICK (goli 3 ndani ya mechi moja)

0 comments:

Post a Comment