Saturday, 13 May 2017

Korea Kaskazini: Tuko tayari kuzungumza na rais Trump

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Korea Kaskazini imesema kuwa itafanya mazungumzo na Marekani iwapo mazigira yataruhusu ,kulingana na vyombo vya habari vya Korea Kusini.
Mjumbe mwandamizi wa Korea Kaskazini amesema kuwa mazungumzo na serikali ya rais Trump yanawezekana kufuatia mkutano na waliokuwa maafisa wa serikali ya Marekani nchini Norway.
Awali mwezi huu rais wa Marekani Donald Trump alisema itakuwa heshima kubwa kukutana na rais Kim Jong un.
Matamshi yake yanajiri kufuatia ongezeko la hali ya wasiwasi kuhusu mipango ya Korea Kaskazini ya kinyuklia pamoja na ile ya utengezaji wa makombora ya masafa marefu.
Choe Son Hui ambaye ni afisa katika wizara ya maswala ya kigeni kuhusu maswala ya Marekani kaskazini alitoa matamshi hayo wakati alipokuwa akirudi Pyongyang baada ya mkutano mjini Oslo.

source:bbc

Related Posts:

  • Takukuru: Tunaendelea Kuwahoji watuhumiwa wa Makinikia TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru imesema kuwa inaendelea kuwahoji watuhumiwa wote walitajwa kwenye sakata la kusafirisha Makinikia ya madini nje ya nchiOfisa Habari wa  (Takukuru), Mussa Misalaba, ames… Read More
  • Mbunge ataka Zitto, Kafulila waombwe radhi kuhusu Sakata la Makinikia Akichangia mjadala huo wa bajeti, Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Ngwali (CUF) alisema wabunge warudi majimboni wakaombe radhi wananchi kwani wao ndiyo walipitisha sheria za madini. “Tuliapa kwa kushika kurani na biblia, kur… Read More
  • Kisa cha Polisi kuwapiga Mabomu ya Machozi Walemavu Dar POLISI jana walitumia mabovu ya machozi kutawanya watu wenye ulemavu waliokuwa wamekusanyika na kufunga barabara ya Sokoine jijini Dar es Salaam.Mabomu hayo yalizua taharuki kwa watumiaji wa njia hiyo na kusababisha usumbuf… Read More
  • ida Kaloli: Nibebeni Mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli amewataka wapenzi wote wa muziki waweze kumbeba ili asipotee tena kama ilivyokuwa hapo awali baada ya kukosa sapoti pamoja na ukosefu wa fedha.Saida amesema baada ya kupata matatizo … Read More
  • Bungeni hapatoshi Sakata la Makinikia BUNGE limeingia siku ya nne jana kujadili Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2017/18, huku wabunge kadhaa wakiraruana kuhusu ripoti ya pili ya kamati iliyoundwa na Rais Dk. John Magufuli, kuhusu mchanga wa dhahabau (makinikia)… Read More

0 comments:

Post a Comment