Saturday, 13 May 2017

Shambulizi la uhalifu wa mtandao laathiri mataifa 99 duniani

Hivi ndivyo ilivyokuwa katika baadhi ya kompyuta wakati wahalifu wa mtandao walipotekeleza shambulio
Sambulizi la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia utumizi wa vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti duniani.
Kampuni ya kulinda uhalifu wa mitandao Avast, imesema kuwa imeona kesi 75,000 za programu zinazotumika kufanya uhalifu mtandaoni inayojulikana kama 'WannaCry' duniani.
Kuna ripoti za maambukizi katika mataifa 99 ikiwemo Urusi nchini China.
Kati ya mashirika yalioathirika zaidi ni shirika la huduma za afya nchini Uingereza na Uskochi.
BBC inaelewa kwamba takriban mashirika 40 na huduma kadhaa za matibabu ziliathirika huku operesheni na mikutano ikifutiliwa mbali.
Programu hiyo ilisambaa kwa kasi siku ya Ijumaa ambapo ilitaka malipo ya dola 300 ili kufungua faili ilizokuwa imeziteka nyara katika kompyuta.
Siku nzima, mataifa ya Ulaya yaliripoti maambukizi hayo.
Idadi kubwa ya kampuni kubwa ikiwemo Telefonica ,kampuni ya umeme ya Iberdrola na ile ya Gesi asilia pia ziliathirika huku kukiwa na ripoti kwamba wafanyikazi katika kampuni hizo waliagizwa kuzima kompyuta zao.
Raia walipiga picha za kompyuta zilizoathirika katika mtandao wa Twitter ikiwemo mashine ya kukata tiketi za safari ya reli nchini Ujerumani pamoja na maabara ya kompyuta nchini Italy.

source:bbc

Related Posts:

  • Majaribio ya ndege mpya za Boeing yasitishwa Shirika la ndege la Boeing limesitisha kwa muda safari za kufanyia majaribio ndege yake mpya ya 737 MAX kutokana na uwezekano wa kasoro kwenye injini za ndege hizo. Hatua hiyo imechukuliwa siku chache kabla ya shirika hil… Read More
  • Mkurugenzi wa kampuni ya ndege apigwa chapati ya uso Australia Hotuba ya mkurugenzi wa shirika la ndege la Australia Airline Qantas ilisitishwa kwa muda baada ya kupigwa na chapati usoni. Alan Joyce alikuwa akihutubia mkutano wa biashara katika eneo la Perth wakati mtu mmoja alipopand… Read More
  • Dawa za kupunguza makali ya HIV Watafiti nchini Uingereza wanasema dawa za kupunguza makali ya virusi katika Ulaya na Amerika ya Kaskazini zimeboreshwa kiasi kwamba watu mwenye Virusi vya UKIMWI wanaweza kuishi kwa karibia sawa tu na watu wengine wasio na… Read More
  • Mafuriko yasababisha shule zote kufungwa Zanzibar Shule zote katika kisiwa cha Zanzibar zimefungwa kwa muda kutokana na mvua kali ambayo imesababisha mafuriko. Waziri wa elimu katika kiswa hicho Riziki Pembe Juma amesema kuwa mvua hiyo ambayo pia imekuwa ikinyesha katika… Read More
  • RATIBA YA LIGI YA AJUCO             AJUCSO MINISRTY OF SPORTS AND ENTERTAINMENT AJUCSO LEAGUE                     &n… Read More

0 comments:

Post a Comment