Saturday, 13 May 2017

Trump amuonya mkuu wa FBI aliyefutwa James Comey

Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump amemtahadharisha mkuu wa shirika la uchunguzi wa jinai FBI aliyefutwa kazi James Comey dhidi ya kufichua habari kwa vyombo vya habari.
Bw Trump ameandika kwenye Twitter kwamba Bw Comey heri "atumai kwamba hakuna kanda zozote kuhusu mazungumzo yetu".
Bw Comey, ambaye amekuwa akiongoza uchunguzi kuhusu uwezekano wa ushirikiano kati ya maafisa wa kampeni wa Bw Trump na serikali ya Urusi alifutwa kazi Jumanne.
Bw Trump baadaye alisema aliambiwa na Bw Comey kwamba yeye mwenyewe hakuwa anachunguzwa.
Bw Trump amesema kwamba alikuwa amehakikishiwa mara mbili na Bw Comey, mara moja wakati wa dhifa ya jioni na mara ya pili kwa njia ya simu kwamba hakuwa anchunguzwa.
Rais huyo amesema: "Nilisema: 'Ikiwezekana, unaweza kunifahamisha: je ninachunguzwa?' Alinijbu: 'Hauchunguzwi.'"
Bw Trump alisema wiki hii kwamba alichukua hatua ya kumfuta Bw Comey mwenyewe.
Wakati wa kumfuta, alimweleza kama mtu asiye wa kuaminika na mtu mwenye kujitakia sifa.
Hilo lilionekana kwenda kinyume na tamko la maafisa wa uatawala wake kwamba Bw Comey alifutwa kutokana na mapendekezo ya Mwanasheria Mkuu jeff Sessions na naibu wake Rod Rosenstein.

Mstari wa kwanza wa barua ya Bw Trump ya kumfuta Bw Comey inarejea barua iliyoandikwa na Bw Rosenstein na inasema: "Nimekubali mapendekezo yao."
Katika ujumbe mwingine kwenye Twitter Ijumaa, Bw Trump alizungumzia tofauti hizo, na kusema: "Mimi ni Rais mwenye shughuli nyingi na shughuli nyingi zinafanyika, haiwezekani kwa watu wangu kusimama jukwaani na kusema jambo kunihusu kwa ufasaha kabisa!"
Aliongeza: "pengine, njia bora zaidi kwangu kufanya inaweza kuwa kwangu kufuta "vikao vya kuwapasha wanahabari" na badala yake niwe nikitoa ujumbe ulioandikwa kwa ajili ya kufanya mambo yote yawe sahihi???"
Bw Trump alipuuzilia mbali uchunguzi unaofanywa na FBI na akasema wafuasi wa Democratic wanatumia "taarifa za uongo" kutuhumu maafisa wake wa kampeni kwamba walikuwa na uhusiano na maafisa wa Urusi.
Aliandika katika ujumbe mwingine: "James Clapper mwenyewe (mkuu wa zamani wa Idara ya Taifa ya Ujasusi), na karibu kila mtu aliyekuwa na ufahamu kuhusu kisa hiki cha kuwinda maafisa wangu, aliposema hakukuwa na uhusiano wowote, ni lini haya yataisha?"
FBI
Mkurugenzi wa zamani wa FBI James Comey
Lakini mrithi wa Comey, kaimu mkuu wa FBI Andrew McCabe, alisema Alhamisi kwamba uchunguzi huo unasalia kuwa "uchunguzi muhimu".
Akitoa ushahidi mbele ya kamati ya Seneti kuhusu ujasusi, aidha, alitilia shaka madai ya ikulu ya White House kwamba Bw Comey alikuwa amepoteza imani machoni pa wafanyakazi wake.
"Ninaweza kuwaambia kwa imani kwamba wengi wa wafafanyakazi wana uhusiano wa ndani na uliokolea na Mkurugenzi Comey," Bw McCabe alisema.
source:bbc

Related Posts:

  • Professa Muhongo amemuibua Kafulila Alikuwa Mbunge Kigoma Kusuni,  David Kafulila ameibuka na kutoa kauli yake maamuzi yaliyofanywa na Rais Magufuli baada ya kupokea ripoti ya Kamati Maalum kuhusiana na uchunguzi wa makontena 272 ya makinikia yaliyokuwa … Read More
  • Ratiba ya Sportpesa Super Cup Sport Pesa Cup 5/6 Singida united Vs FC leopardYanga Vs Tusker fc6/5 Simba Vs Nakuru All StarJang`ombe boys vs Gor mahiaNusu fainali tarehe 8Bingwa wa mechi kati ya Singida united vs AFC leopard atacheza na bingwa kati ya… Read More
  • Trump asababisha Al Jazeera kufungiwa Saudi Arabia Saudi Arabia imeifungia mitandao ya Al Jazeera na Magazeti ya Qatar baada ya Rais wa Qatar Tamim Bin Hamad Al-Thani kusema anaishangaa Saudi Arabia kumkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump kauli iliyopingwa na Mfalme wa … Read More
  • Nikki wa Pili ampongeza Rais Magufuli Msanii wa Nikki wa Pili, amempongeza Rais Magufuli kwa kitendo alichokifanya leo cha kumtumbua Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo na kumwambia Mungu amsimamie katika kupambana na ufisadi.Niki ameto… Read More
  • Kutana na Msikiti unaojengwa ila mafundi hawaonekani Uliwahi kusikia jengo linalojengwa kwa muda mrefu zaidi na mafundi hawaonekani, iwe usiku au mchana jengo linazidi kupanda juu, pia ata magari ya kubeba kokoto, mchanga hata matofari yasionekane...!!! Hii ni mpya kutok… Read More

0 comments:

Post a Comment