Sunday 21 May 2017

Libya yakabiliwa na vita vya ndani

Libya
Taarifa kutoka nchini Libya zinaelez kwamba jeshi liloljitangaza kuwa la taifa hilo, ambalo linaunga mkono mamlaka yenye makao yake katika mji wa mashariki wa Tobruk,limefanya mashambuliuzi kadhaa ya anga dhidi ya vikosi pinzani ambavyo ni waaminifu kwa serikali inayotambulika kimataifa iliyoko katika mji mkuu wa Libya.
Mashambulizi saba ya anga yameripotiwa kutekelezwa , yakilenga zaidi miji ya Hun na Jafra iliyoko Kusini mwa Libya mwishoni mwa juma lililopita nyakati za usiku, yakihusishw apia na shambulizi la ulipizaji kisasi wa kikosi cha anga cha LNA mnamo siku ya Alhamisi juma lililopita.
Mashuhuda wa mashambuli hayo wanaliambia shirika la Human Rights Watch kwamba, miongoni mwa watu thelathini waliouawa katika eneo hilo walikuwa na majeraha ya risasi vichwani mwao na baadhi ya maiti zilikuwa zimefungwa mikono.
Shambulizi hili lina lina zuia taarifa za ukweli wa mambo baina ya majeshi ambayo ni pande mbili hasimu zilizoanza kuzidi kuhasimiana mwanzoni mwa mwaka huu.
wakati huo huo
Mkuu wa umoja wa mataifa anaye shughulikia kitengo cha wakimbizi amesema kwamba wote wanaotafuta hifadhi na wakimbizi nchini Libya wanapaswa kuondolewa vizuizini na kupewa usaidizi mwingine.
Akiwa katika ziara yake mjini Tripoli, Filippo Grandi, amesema kwamba ameridhishwa na ulinzi unaotolewa na serikali lakini ameshtushwa na hali mbaya waliyonayo wakimbizi na wahamiaji mahali wanakoshikiliwa.
Libya bado inasalia kuwa ndiyo eneo pekee ama kituo kikuu kinachotumiwa na wakimbizi kwenda katika nchi walizozidhamiria ikiwemo Syria kwa matumaini ya kwenda barani Ulaya.
Kitengo hicho cha umoja wa mataifa kinachoshughulika na wakimbizi kimeeleza kwamba kimechukua hatua ya kuonesha uwepo wake na kuweka mipango ya kukabiliana na
hali mbaya kutokana na mgogoro huo.



source:bbc

0 comments:

Post a Comment