Monday 22 May 2017

MAAJABU:Mchoro wauzwa kwa $110.5m Marekani

Mchoro wa msanii Jean Michel Basquiat umeauzwa katika mnada mjini New York kwa takriban dola milioni 110.5.Haki miliki ya pichaYUSAKU2020, INSTAGRAM
Image captionMchoro wa msanii Jean Michel Basquiat umeauzwa katika mnada mjini New York kwa takriban dola milioni 110.5.
Mchoro wa msanii Jean Michel Basquiat umeauzwa katika mnada mjini New York kwa takriban dola milioni 110.5.
Hiyo ni mara mbili ya bei ya mchoro kama huo wenye thamani kubwa kununuliwa na mtu huyo huyo mwaka uliopita.
Ulivunja rekodi kadhaa ikiwemo kuwa mchoro wenye thamani kubwa kuwahi kuchorwa na mchoraji yoyote nchini Marekani.
Pia ni pato kubwa kuwahi kupewa msanii mweusi na wa kwanza tangu 1980 kuvunja rekodi ya dola milioni 100.
Mchoro huo usio na jina ulichorwa katika fito zenye mafuta, akriliki na rangi, una fananisha uso wenye umbo la fuvu.
Mchoro huo ulinunuliwa na Yusaku Maezawa, mfanyibiashara wa fesheni mwenye umri wa miaka 41 ambaye ana mpango wa kuanzisha jumba la makumbusho katika mji wake wa nyumbani wa Chuba.
Aliwania mchoro huo wakati wa mnada uliofanyika Sotheby uliochukua takriban dakika 10.
Kulikuwa na furaha nderemo na vigelegele katika mnada huo wakati mchoro huo ulipouzwa kwa Maezawa kwa simu.
Baadaye aliweka chapisho katika mtandao wake wa Instagram kwamba mchoro huo ulimfanya kujihisi kuwa na furaha kubwa na shukran kwa kuwa mpenzi wa uchoraji.
Mwaka uliopita Bwana Maezawa aliweka rekodi mpya kwa mchoro wa Basquiat wakati alipolipa dola milioni 57.3 kwa mchoro wa shetani mwenye pembe.

source:bbc

0 comments:

Post a Comment