Monday, 22 May 2017

Mgahawa wakumbwa na habari bandia za kuuza ''nyama ya binadamu''

Mkahawa wakumbwa na habari bandia za kuuza ''nyama ya binadamu''
Image captionMkahawa wakumbwa na habari bandia za kuuza ''nyama ya binadamu''
Mgahawa mmoja mjini London umekumbwa na habari bandia za kuuza nyama ya mtu.
Wafanyiakazi katika mgahawa wa Karri Twist katika eneo la New Cross nchini Uingereza wamehangaishwa kwa kupigiwa simu kutoka kwa wateja wanaosema ''Kwa nini hamujafunga''?.
Mgahawa huo wa chakula cha jioni ni mwathiriwa wa habari za mzaha zilizodai kwamba mmiliki wake alikamatwa kwa kuweka nyama ya binadamu katika chakula na kwamba miili 9 ilipatikana katika jokovu la mgahawa huo.
Na watu wengine waliamini mzaha huo.
Habari hiyo ilichapishwa katika chombo cha habari cha channel23news.com, mtandao ambao wateja wake wanaweza kuchapisha habari za uwongo ili kuwafanyia mzaha rafiki zao kwa kuchapisha moja kwa moja katika mtandao wa fecbook.
Shinra Begum ambaye ndio mmiliki wake aliambia Newsbeat kwamba biashara hiyo ya familia imekumbwa na wakati mgumu tangu habari hiyo ilipochapishwa siku ya Alhamisi.
''Wakati watu walipoanza kunipigia simu na kuuliza iwapo tulikuwa tukiuza nyama ya binadamu sikuamini''.
''Nilishtuka nilipoaana habari hiyo katika mtandao na kuendelea kusambazwa katika mtandao wa facebook''.
Sasa watu wametishia kulivunja jengo letu na nimelazimika kuketi chini na mteja ili kumuelezea kwamba yote hayo ni madai ya uwongo.
Shinra anasema kuwa alilazimika kuripoti kwa maafisa wa polisi kwa sababu lilikuwa swala lililomtia wasiwasi mkubwa.
Njia ya pekee ambapo Karri Twist iliweza kukabiliana na chuki hiyo ni kupitia kuchapisha katika mtandao wao ili kuhakikisha kwamba watu wanajua kwamba hilo halikuwa la kweli.


SOURCE:BBC

Related Posts:

  • Nchemba amtolea uvivu Tundu Lissu  Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ‘amemvaa’ Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kwamba amejaribu kutengeneza kila aina ya kichaka kukwamisha jitihada za Rais John Magufuli kupambana na usafirish… Read More
  • Ole Sendeka atuma salamu hizi kwa Lowassa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amempongeza Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kumpongeza Rais John Magufuli kufuatia uamuzi aliouchukua kuhusu mchanga wa madini yanayochimbwa nchini na kampuni ya Ac… Read More
  • Simba yatumia Mil. 100/ kumshawishi Niyonzima NI UMAFIA TU! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima kudaiwa kujiunga na Klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kupewa ofa ya Sh. milioni 100. Habari zilizopatikana jana jioni … Read More
  • Ally Mayay, Mtemi kuwania urais TFF  MAYAY Ally Mayay anatarajia kuchukua nafasi ya kuwania Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).Taarifa zinaeleza Mayay ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, atachukua fomu hizo leo. MTEMI Wa… Read More
  • Hoja 6 moto mkali kwa serikali bungeni MJADALA wa mapendekezo ya makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 unatarajiwa kuhitimishwa leo mjini hapa huku hoja sita zikionekana kuwa mtihani mgumu kwa serikali kuzitolea majibu kesho wakati in… Read More

0 comments:

Post a Comment