Mwanamume mmoja katika jimbo la Texas, Marekani anadaiwa kuwashtaki mwanawake ambao aliyekuwa amemlipia wakatazame sinema walipokuwa wanachumbiana lakini akaanza kutumia simu yake kutuma ujumbe kwa mtu mwingine.
Kwa mujibu wa gazeti la Statesmen, Brandon Vezmar, 37, anataka alipwe fidia ya $17.31 (£13.38), ambayo ni thamani ya tiketi alizowalipia wanawake hao wakatazame filamu ya Guardians of the Galaxy Vol. 2.
"Ilikuwa kama kikao cha kwanza cha kuchumbiana kutoka jehanamu," alisema.
Anasema alikutana na mwanamke huyo mtandaoni.
Mwanamke huyo wa miaka 35, ambaye hawezi kutajwa jina, anasema hajafahamu kufikia sasa kuhusu ombi la mwanamume huyo, lakini ameongeza kwamba ni la kushangaza mno.
Brandon anadai kwamba dakika 15 baada yao kuanza kutazama filamu, mwanamke huyo alianza kutuma ujumbe kwa kutumia simu yake.
Kwenye kesi aliyowasilisha mahakamani Travis, mwanamume huyo anadai mwanamke huyo alitumia simu "angalau mara 10-20 katika kipindi cha dakika 15."
Baada yake kumuomba aende akatumie simu nje ya ukumbi wa sinema, Brandon anasema mwanamke huyo aliondoka na kwenda zake kabisa na hakurejea.
Mwanamke huyo hata hivyo anasema alitumia simu mara mbili au tatu pekee, na kwamba alikuwa anamwandikia ujumbe rafiki yake wa kike ambaye alikuwa amekorofishana na mpenzi wake wa kiume.
Mwelekezi wa filamu hiyo James Gunn ameingilia kati.
Ameandika kwenye Twitter kwamba mwanamke huyo anafaa hata kufungwa jela.
Mwanamke huyo naye amesema atamchukulia hatua za kisheria Brandon Vezmar kwa kuwasiliana na dadake mdogo akidai pesa hizo.
"Mimi si mwanamke mfidhuli," anasema.
"Nilienda tu kwa kikao cha kuchumbiana."
source:bbc
0 comments:
Post a Comment