Monday, 22 May 2017

Marufuku ya uuzaji wa nyama ya mbwa yasababisha wasiwasi China

Marufuku ya uuzaji wa nyama ya mbwa yazuia wasiwasi katika hafla ya Yulin China
Sherehe ya kula nyama ya mbwa nchini China ilio na umaarufu kwa ukatili wa wanyama mwaka huu itapigwa marufuku kuuza nyama ya mbwa.
Ulaji wa mbwa nchini China sio haramu na wauzaji wa nyama hiyo tayari wameanza kulalamikia marufuku hiyo wengine wakisema hawajaisikia .
Sherehe hiyo inayofanyika mwezi Juni kila mwaka imekuwa ikivutia pingamizi kubwa kutoka kwa wanaharaki wa wanyama wanaosema kuwa wanyama hao hufanyiwa ukatili.
Inakadiriwa kuwa katika sherehe hiyo ya Yulin iliofanyika miaka michache iliopita, takriban mbwa na paka 10,000 walichinjwa na kufanywa kitoweo wakati wa sherehe hiyo ya siku kumi.
Lakini idadi hiyo imekuwa ikipungua katika siku za hivi karibuni huku pingamizi ikiendelea nchini China na kimataifa.
Wanaharakati kadhaa wa wanyama wanasema kuwa wauzaji na mikahawa wameambiwa kwamba hakuna nyama ya mbwa itakayouzwa wakati na kabla ya sherehe hiyo.
Peter Li, mtaalamu wa sera za China aliambia BBC kwamba mamlaka tayari imejaribu kuwakatisha tamaa wanaotekeleza hatua hiyo ,na kwamba mwaka huu itawapiga faini watakaokiuka marufuku hiyo.
Raia wa China wakila nyama ya mbwa wakati wa sherehe ya Ylin nchini humoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRaia wa China wakila nyama ya mbwa wakati wa sherehe ya Ylin nchini humo
Sheria hiyo itaathiri wauzaji wa nyama ya mbwa, wafanyibiashara na wenye mikahawa.
Lakini marufuku hiyo itakuwa ya muda ikimaanisha kwamba mbwa wengi wanaweza kuchinjwa kabala ya sherehe hiyo.
''Bado kuna pingamizi kutoka kwa wafanyibiashara wa nyama hiyo ya mbwa'', alisema bwana Li.
''Kote nchini walikuza ulaji wa nyama ya mbwa kama utamaduni wa kitaifa pamoja na chakula cha Wachina.
Hilo sio la kweli ,baraza la mji wa Yulin haliweza kufanya kitu kama hicho kwa kuwa kitasababisha wasiwasi mkubwa kwa kijamii.
source:bbc

Related Posts:

  • DIPLOMA AJUCO WAICHAPA SECOND YEAR AJUCOLigi ya AJUCO (inter class) imeendelea leo  katika viwanja vya RMA ambapo mechi nne zilichezwa na mechi ya kwanza ilichezwa kati ya AJUCO second year na AJUCO diploma majira ya saa nane mchana. Lakini kwa upande w… Read More
  • AJUCO THIRD YEAR WATUNISHIWA MISULI NA RMA Katika kile ambacho hakikutarajiwa na mashabiki wengi wa AJUCO third year lakini kimewezekana ni baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya timu ya chuo cha wauguzi Songea maarufu kama RMA. Mechi hiyo ilichezwa katika… Read More
  • MWAKA WA TATU WAKUBALI KIPIGO TENAIkiwa ni mwendelezo wa michuano ya AJUCO ligi (inter class), leo hii majira ya jioni hali imekuwa mbaya kwa wakongwe wa chuo cha AJUCO (third year) baada ya kukubali kipigo cha magoli 3-2 kutoka kwa wadogo zao mwaka wa kwanza… Read More
  • Mwanamke ajioa baada ya kukosa mchumba Q May Chen Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa Mwanamke mmoja ambaye anaugua saratani ya matiti amejioa mwenyewe baada ya kusubiri mc… Read More
  • Jambazi wa kike auawa na polisi Nairobi Mwanamke anayedaiwa kuwa jambazi sugu, ambaye amekuwa akipakia mtandaoni picha zake akiwa amejipodoa na kujipamba, ameuawa na polisi jijini Nairobi. Kijana huyo ambaye ametambuliwa kama Claire Mwaniki aliuawa na polisi alf… Read More

0 comments:

Post a Comment