Tuesday 23 May 2017

Madhara ya Mvua ya siku sita yaua 10, yabomoa nyumba 44

Tanga. Tathmini ya madhara yaliyotokana na na mvua zilizonyesha kwa siku sita mfululizo wiki iliyopita mkoani hapa zimeonyesha kuwa hadi sasa watu 10 wamekufa huku  nyumba 44 zikibomoka na nyingine 218 zikizingirwa na maji.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba ametoa  taarifa

ya tahmini hiyo leo, Jumanne wakati akizumgumza na waandishi wa habari jijini hapa.

Wakulyamba amesema katika yaliyotokena na mvua hizo, watu 10 walimepoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko, kuangukiwa nyumba na kutumbukia kwenye mashimo  ambapo  saba kati yao  walikuwa wakazi wa Wilaya ya Korogwe, wawili Muheza na mwingine ni mkazi wa Jiji la Tanga huku 20  wakijeruhiwa.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, nyumba 44  ziliezuliwa paa, 218 zilizingirwa na maji, 12 zikisombwa na mafuriko.

Amesema wilaya zilizoathirika zaidi ni Korogwe,Tanga na Lushoto huku Pangani,Mkinga

na Handeni zikipata athari  ndogo.

Kamanda huyo alisema katika mafuriko hayo,barabara zilizopo katika za Wilaya mbalimbali mkoani Tanga,zimeathirika kwa kubomoka,kuvunjika makaravati pamaoja na madaraja.

"Kama mnavyoona mvua bado zinaendelea, nawatahadharisha wanaokaa kwenye nyumba zilizopo mabondeni wasisubiri maji yaingie ili waokolewe, kuna wakati mwingine uokoaji unaweza kutofanikiwa na kujikuta mnaangamia,"amesema Wakulyamba.

source:mtanzania

0 comments:

Post a Comment