Korea Kusini inasema kuwa imekishambulia ''kifaa'' kutoka Korea Kaskazini kilichorushwa katika eneo lisilo la kijeshi.
Takriban risasi 90 zilifyatuliwa zikielekezwa kwa kifaa hicho ambacho kufikia sasa hakijajulikana kilikuwa nini hasa.
Korea Kaskazini imerusha ndege zisizokuwa na rubani katika mpaka huo siku za hapo awali.
Katika taarifa, jeshi la Korea Kusini limesema kuwa jeshi lake linaweka ulinzi mkali.
Kisa hicho kinajiri wakati ambapo kuna wasiwasi mkubwa katika rasi ya Korea.
Siku ya Jumapili Pyongyang ilitekeleza kile ilichodai kuwa jaribio lililofanikiwa la kombora la masafa ya kadri.
Jaribio hilo linajiri wiki moja baada ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kile ilichodai kuwa ni kombora jipya linaloweza kubeba kichwa cha nyuklia, ambalo lina uwezo wa kushambulia Marekani.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya kikao cha faragha kuhusu Korea Kaskzini siku ya Jumanne jioni.
Katika taarifa siku ya Jumatatu ,lilikubali kuchukua hatua muhimu ikiwemo vikwazo ili kuishinikiza Korea Kaskazni kusitisha hatua yake .
Ongezeko hilo la wasiwasi linajiri wakati ambapo kuna rais mpya Korea Kusini .
Moon Jae alikula kiapo cha kuchukua mamlaka mapema mwezi huu baada ya mtangulizi wake Park Geun Hye kushtakiwa.
Kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi.
Bwana Moon anapendelea majadiliano na Korea Kaskazini ikilinganishwa na mtangulizi wake.
Maafisa wa Korea Kusini hawakusema iwapo walikishambulia ama kukikamata kitu hicho kilichorushwa katika eneo hilo ambalo ni marufuku kwa shughuli zozote za kijeshi lakini visa kama hivyo vimetokea hapo awali.
Mnamo mwezi Januari 2016 wanajeshi waliopo mpakani mwa Korea Kusini waliishambulia ndege moja isiokuwa na rubani.
Mnamo 2014, maafisa wa Korea Kusini walisema kuwa walipata ndege mbili zisizokuwa na rubani katika eneo ambalo ni marufuku kwa shughuli za kijeshi karibu na Paju na nyengine katika kisiwa karibu na eneo linalozozaniwa la baharini kati ya mataifa hayo ya Korea.
Tuesday, 23 May 2017
Home »
» Korea Kusini yashambulia kifaa cha Korea Kaskazini
Korea Kusini yashambulia kifaa cha Korea Kaskazini
Related Posts:
Mbunge Peter Serukamba asema Rais Magufuli ataigwa duniani kote Mbunge wa Kigoma Vijijini (CCM), Peter Serukamba amefunguka na kusema jambo alilofanya Rais Magufuli kuzuia mchanga litakwenda kuigwa duniani kote na kuleta mapinduzi katika 'Extractive Industries' kwa kazi kubwa aliyofan… Read More
Upepo mkali watarajiwa kuvuma pwani ya Tanzania Image captionWanaotumia bahari wametakiwa kuchukua tahadhari Tanzania Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa tahadhari ya kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya pwani ya Tanzania. Maeneo yanayotarajiwa… Read More
Mbunge Peter Serukamba asema Rais Magufuli ataigwa duniani kote Mbunge wa Kigoma Vijijini (CCM), Peter Serukamba amefunguka na kusema jambo alilofanya Rais Magufuli kuzuia mchanga litakwenda kuigwa duniani kote na kuleta mapinduzi katika 'Extractive Industries' kwa kazi kubwa aliyofan… Read More
SAKATA LA MCHANGA WA MADINI, NGOMA BADO MBICHI MWENENDO wa sakata la kusafirisha mchanga wa madini nje ya nchi, umeonyesha kila dalili kwamba huenda suala hilo sasa likachukua muda mrefu zaidi. Tangu kamati ya wataalamu wa sayansi iliyoundwa kuchunguza kiwango cha madi… Read More
Hali tete:Mkuu wa mawasiliano White House aacha kaziHaki miliki ya pichaBLACK ROCK GROUPImage captionMike Dubke alitazamwa kama mtu wa kutoka nje White House Mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu ya White House amejiuzulu miezi mitatu pekee baada yake kupewa kazi hiyo na Rais… Read More
0 comments:
Post a Comment