Monday, 15 May 2017

Microsoft: Shambulizi la Kompyuta liwe funzo

Shambulizi la mitandaoni laathiri mataifa 150
Shambulizi la uhalifu wa mitandaoni lililoathiri mataifa 150 tangu siku ya Ijumaa linafaa kuchukuliwa kama funzo, Microsoft imesema.
Kampuni hiyo ya kompyuta inasema kuwa hatua ya serikali hizo kutoimarisha programu zao mara kwa mara ndio sababu ya tatizo hilo.
Kirusi hicho kilichukua fursa ya dosari ya toleo la programu ya Microsoft Windows lililogunduliwa na majasusi wa Marekani.
Kuna hofu ya shambulio jingine la kirusi hicho cha 'ransomware' huku raia wakitarajiwa kurudi kazini siku ya Jumatatu.
Kampuni nyingi zimeajiri wataalam waliofanya kazi wikendi kuzuia maambukizi mapya.
Kirusi hicho kiliteka faili na kutaka kulipwa dola 300 kama kikombozi.
Kusambaa kwa kirusi hicho kulipungua wikendi lakini huenda hali hiyo ikawa ya muda ,wataalam wameonya.
Zaidi ya Komyuta 200,000 zimeathiriwa kufikia sasa.
Taarifa kutoka kwa rais wa Microsoft na afisa mkuu wa maswala ya sheria Brad Smith siku ya Jumapili ilikosoa vile serikali zinavyoweka taarifa zao kuhusu dosari za kiusalama katika mifumo ya kompyuta.
''Tumeona dosari zinazohifadhiwa na CIA zinaonekana katika Wikileaks na sasa dosari ilioibwa kutoka kwa NSA imeathiri wateja kote duniani'', aliandika
''Ukilinganisha na silaha za kisasa hiyo inamaanisha kwamba Silaha za Marekani kama vile Tomahawk zingekuwa zimeibwa''.
source:bbc

Related Posts:

  • Mwanasheria Mkuu wa TBS Afikishwa Mahakamani Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco (54) amepandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu ya kuishi na kufanya kazi nchini bila kuwa na  kibali.Mwendesha Mashtaka w… Read More
  • Dkt Mpango awasilisha taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2016 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango. Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewasilisha taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2016 na Mpango wa maendeleo ya uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2017/2018. Akiwa… Read More
  • Wakamatwa na dawa za kulevya Mwanza Jeshi la Polisi Mwanza linawashikilia watu wanne baada ya kuwakuta na dawa za kulevya aina ya Mirungi mafungu 57 yenye ukubwa wa kilogramu 56.75 ambayo yalikuwa yamewekwa kwenye mabegi na magunia.Kamanda wa Polisi Mwanza, A… Read More
  • Ester Bulaya asema: Hamjatuziba midomo Mbunge wa Bunda Mjini Mh. Ester Bulaya ametoa salamu kwa Wabunge wa CCM pamoja na Spika Job Ndugai kutambua kwamba hata baada ya kumuadhibu kutohudhuria vikao bya bunge siyo silaha ya kuwafunga midomo.Bulaya amefunguka hayo… Read More
  • Qatar yaapa kutosalimu amri mzozo wake na nchi za KiarabuHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionSaudi Arabia na nchi nyingine kadha za Kiarabu zimesitisha safari za ndege kuingia na kuondoka Qatar Qatar imeapa kwamba haitasalimu amri katika mzozo wake kuhusu sera yake ya kigeni na… Read More

0 comments:

Post a Comment