Thursday 18 May 2017

NI ZAIDI YA SIASA:Trump aunga mpango wa kinyuklia wa Iran aliodai ''kuwa mbaya''

Rais Trump ameongeza makubaliano ya mpango wa kinyuklia kati ya Marekani na Iran
Rais Trump ameongeza makubaliano ya mpango wa kinyuklia kati ya Marekani na Iran
Ikulu ya Whitehouse nchini Marekani imeendeleza mpango wa kuipunguzia vikwazo Iran licha ya rais Donald Trump kuukosa mpango huo.
Kuondolewa kwa vikwazo ni miongoni mwa makubaliano ya kinyuklia yalioafikiwa 2015 chini ya aliyekuwa rais Barrack Obama pamoja na mataifa mengine matano yenye uwezo mkubwa duniani.
Bwana Trump ameelezea makubaliano hayo kuwa mabaya zaidi.
Hatahivyo wizara ya fedha nchini humo iliwawekea vikwazo maafisa fulani na mfanyibiashara wa China anayehusishwa na mpango wa makombora wa Iran.
Hatua hiyo inamaanisha vikwazo vinavyozuia kampuni zozote za Marekani zinazoiuzia ama kushirikiana na Iran vitaendelea kulemazwa.
Kwa upande wake Iran imekubali kupunguza mipango yake ya nyuklia, kupunguza uhifadhi wa madini ya Uranium, uzalishaji wa Plutonium na kuwaruhusu wachunguzi kuchunguza vifaa vyake.
Vikwazo vipya kutoka kwa wizara ya fedha vinaathiri watu binafsi wakiwemo maafisa wawili wa Iran katika idara ya ulinzi na wanaouza makombora ya kijeshi ili kulipiza kisasai jaribio la kombora pamoja na hatua ya Iran kumuunga mkono Bashar al-Assad wa Syria.
Raia wa Marekani na washirika wake sasa hawaruhusiwi kuingia mikataba na maafisa hao na kampuni husika.
SOURCE:BBC

0 comments:

Post a Comment