Binti wa mfalme nchini Japan, Mako, ameamua kuacha maisha ya kifalme kwa ajili ya mapenzi.
Binti wa mfalme nchini Japan, Mako, ameamua kuacha maisha ya kifalme kwa ajili ya mapenzi.
Hii ni baada ya mwanamfalme Mako, ambaye ni mjukuu wa mfalme Akihito, kukubali kuoana na Kei Komuro ambaye ni mwananchi wa kawaida nchini mwao.
Wawili hao walipendeana baada ya kukutana katika hoteli moja mnamo mwaka wa 2012.
Mwanamfalme Mako mwenye umri wa miaka 25, atafunga ndoa na mfanyikazi wa kampuni ya mawakili, Kei Komuro waliosoma pamoja katika chuo cha Christian University mjini Tokyo.
Sheria za kifalme nchini Japan zinamhitaji yeyote atakayeoana na mtu asiyetoka kwenye kasri, aache ufalme.
Ufalme wa Japan umethibitisha kuwa mipango ya harusi inaendelea lakini itatangazwa rasmi baada ya tarehe rasmi kujulikana.
Hata hivyo, Bw Komuro amedinda kuzungumzia mipango ya harusi. ''sio wakati mwakafaka wa kuzungumza, nitasema muda ufaao,'' alisema.
Hatua hiyo imezua gumzo nchini Japan kuhusu urithi wa ufalme huku mfalme Akihito akikaribia kustaafu.
Hii sio mara ya kwanza hilo kutokea, kwani shangaziye Princess Mako, ambaye pia ni binti pekee wa mfalme akihito, Princess Sayako, alilazimika kuondoka kasrini baada ya kuoana na mpenzi wake mwaka wa 2005.
Alilazimika kujifunza maisha ya kawaida, ikiwemo kuendesha gari na kufanya ununuzi wa bidhaa za nyumba.
Mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita, Mfalme Akihito mwenye umri wa miaka 83, alidokeza kustaafu kwake kutokana na umri wake.
source:bbc
0 comments:
Post a Comment