Friday 5 May 2017

Siri ya kufaulu mtihani: Mmea wa Rosemary husaidia kukumbuka mambo

rosemary
Watafiti nchini Uingereza wamesema huenda harufu ya mmea wa rosemary ikawa na uwezo wa kusaidia mtu kukumbuka mambo.
Mmea huyo, ambao huwa na maua ya rangi ya nyeupe, waridi, zambarau au samawati, sana hutumiwa kama kiungo kwenye chakula, vinywaji au mchuzi.
Utafiti ulibaini kwamba wanafunzi waliokuwa kwenye chumba kilichopulizwa harufu ya rosemary, iliyokuwa kwenye mafuta, walikuwa na uwezo wa kukumbuka mambo kwa asilimia 5 hadi 7 zaidi kuliko wanafunzi ambao hawanusa harufu hiyo.
Mark Moss kutoka Chuo Kikuu cha Northumbria anasema matokeo ya kutumia mmea huyo yalikuwa sawa pia kwa watu wazima.
Dkt Moss alisema utafiti huo unaonekana kutilia mkazo itikadi kuhusu uwezo wa mmea huo.
Amesema kwa miaka mingi, mmea huyo umehusishwa na uwezo wa kukumbuka mambo.
SOURCE: BBC

0 comments:

Post a Comment