Friday 5 May 2017

Hali yazidi kuwa tata Korea Kaskazini: CIA wanapanga kumuua Kim Jong-un

Maajenti wa Marekani na Korea Kusini wanapanga njama ya kumuua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, vyombo vya habari nchini humo vimesema.
Taarifa kutoka wizara ya usalama nchini Korea Kusini imesema mawakala wa kundi la kigaidi linaloungwa mkono na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na shirika la ujasusi la Korea Kusini wameingia nchini Korea Kusini wakiwa na silaha hatari ya bio-kemikali.

Taarifa hiyo imesema Korea Kaskazini itawasaka mawakala hao na kuwaangamiza bila huruma.Ikumbukwe kuwa uhasama kati ya Marekani na korea Kaskazini haujaanza leo, bali ulianza miaka mingi sana.

SOURCE: BBC

0 comments:

Post a Comment