TAASISI isiyo ya Kiserikali ya TOWSF inayojihusisha na kusaidia wanawake wajane na watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi yenye ofisi zake katika Wilaya mpya ya Kaliua Mkoa wa Tabora nchini Tanzania tangu ianze kazi mwaka 2013 imeshawafikia walengwa zaidi ya 1,000.
Mwenyekiti wa taasisi hiyo Taifa Imani Matabula alisema kuwa malengo ya kuanzishwa kwake haswa ni kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi sanjali na akina mama wajane ambao wamefiwa na waume zao hivyo baada ya kubaini changamoto hizo wakaamua kuanzisha taasisi hiyo.
Alisema kuwa wilaya hiyo familia kadhaa zimepoteza wazazi au wakezi hivyo kusabasha kuyumba hivyo kuongeza watoto waishio katika mazingira magumu na wajane, huku akisema takwimu ya mwaka 2012 ya sensa, wilaya ilikuwa na wakazi 39,000, na kwamba kuna kasi ya ongezeko la ugonjwa wa Ukimwi hivyo kuongezeka kwa wajane na watoto waishio katika mazingira hatarishi.
"Taasisi ilianzisha jijini Dar es Salaam kwa malengo ya kupambana na makundi hayo, mimi ni mzawa wa Kaliua, kutokana na changamoto inayowakabili wakazi wenzangu hususani watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi na akinamama waishio katika mazingira hataridhi, nikaona kuna umuhimu wa kuwepo na tawi hapa," alisema Matabula.
Aliwapongeza wazee maarufu wilayani humo baadhi yao Hamisi Madili, Alfred Lucas Mpulani, Juma Salehe na Salumu Matongo na wengine kadhaa ambao baada ya kuwafikishia wazo hilo walilipokea vizuri kisha kuwaongezea ushauri ambao umefanikisha kuanzishwa kwa tawi hilo.
"Taasisi imeanza mwaka 2013 ina vyerehani vitano, vitatu vipo Dar es Salaam, viwili hivi hapa, tuna miaka minne, tumewafikia walengwa 1,000, dhamira yetu wajane wote wanaondokana na utegemezi, pia tuna wanafunzi waliokwenda kidato cha tano na sita, na walioingia vyuo vikuu ambao ni zao la taasisi na ndani ya miaka mitatu watakuwa na kaya si chini ya 30. " alisema Matabula.
Alisema kipaumbele ni elimu, na kwamba familia nyingi zinazopoteza wazazi au walezi wanakosa huduma stahiki hivyo kupelekwa kwenye vituo vinavyolelea yatima hali inayokosesha haki za msingi za kusoma na kuwa wana orodha ya wanafunzi 438 wanaopatiwa huduma na taasisi pasipo kuchangia kitu chochote.
"Katika msimu uliopita tumekabidhi wanafunzi madaftari 10 kila mmoja sanjali na sare kwa wanafunzi 80, wito wangu tunaiomba Serikali na wadau wa maendeleo kuitupia macho taasisi hii inayodhamiria kupambana na changamoto hizo ili walengwa wapate kile wanachokihitaji," alisema.
Fundi Mkuu anayewafundisha walengwa hao Elovida Kasitu alisema kuwa anawafundisha wajane pamoja na yatima na kwamba wengi wanawaleta watoto na hiyo inatokana na wahusika wengi kiwana umri mkubwa hivyo kushindwa kujihusisha na shughuli hiyo na kuwa vijana wanayapokea vizuri mafunzo, huku akisema wengi wao kuanzia umri wa miaka 18 mpaka 40.
"Changamoto inayotukabili ni kuwepo kwa vitendekazi vichache ambavyo vinatunyima fursa pana ya kutimiza majukumu yetu, tunaiomba Serikali na wadau wa maendeleo waelekeze jicho katika taasisi hii kwani inalengo la kuiendeleza jamii ya hapa Kaliua," alisema Mwalimu huyo.
Asia Juma Rajabu mmoja wa wanafunzi aliyemaliza kidato cha nne ametoa wito kwa jamii ya Kaliua kutoa ushirikiano kwa viongozi wa taasisi ili malengo yao yaweze kutimia na kwamba wamedhamilia kuwakomboa wananchi wa eneo hilo.
"Nimemaliza kidato cha nne mwaka jana nimepata cheti, naiomba jamii ibadilike ielekeze nguvu zaidi katika elimu sanjali na kusaidia viongozi wa taasisi ambao wameleta ofisi hapa kwa nia ya kutusaidia sisi wenyewe," alisema Asia.
Salumu Matombo alisema kuwa ni wakati mwafaka kwa viongozi wa Halmashauri kielekeza nguvu katika kusukuma maendeleo ya taasisi hiyo ambayo imedha,ilia kuwakomnoa wana-Kaliua kutokana na changamoto zinazowakabili.
source:muungwana
0 comments:
Post a Comment