Wakuu wa biashara wa Korea Kusini wanasema, Uchina imeiuzia Korea Kaskazini magari, televisheni, na simu za mkononi nyingi zaidi mwaka jana, ikionyesha kuwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa haivikuathiri mahitaji ya Korea Kaskazini kwa bidhaa hizo.
Data za Korea Kusini, zinaonyesha kuwa mauzo ya televisheni kutoka Uchina kwa Korea Kaskazini, yameongezeka zaidi ya asilimia mia moja katika mwaka mmoja, baada ya Korea Kaskazini kuanzisha utangazaji wa kidijitali.
Na mauzo ya simu pia kutoka Uchina, katika miezi mitatu ya awali mwaka huu, yalizidi dola milioni 25 zaidi ya mara dufu kushinda kipindi kama hicho mwaka jana.
Uchina imeacha kununua makaa kutoka Korea Kaskazini, kufuatana na vikwazo vya Umoja wa Mataifa, lakini inaendelea kusaidia uchumi wa huko kukua taratibu.
0 comments:
Post a Comment