Sunday, 4 June 2017

Neno lingine la J.Kikwete kwa Rais Magufuli: JPM

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefunguka na kusema suala la kuongoza nchi ni kazi kubwa mno na kusema yeye toka amestaafu kazi hiyo saizi anaweza kulala na usingizi ukaisha vizuri lakini kipindi cha nyuma haikuwa hivyo.

Kikwete amesema hayo jana kwenye Futari maalumu iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi nyumbani kwake Msoga, Pwani na kusema saizi mzigo huo ameubeba Rais Magufuli na kudai huwa anamtia moyo kuwa anapaswa kupambana kwani hata wao wamepitia mambo ambayo yeye anapitia. 

"Sasa nimestaafu muda wa kuwasaidieni ninao tofauti na zamani, zamani mambo mengi kubeba mzigo wa kuongoza nchi kazi kubwa sana saizi anahangaika nao Rais Magufuli wakati mwingine nampa moyo tu bwana wewe pambana, wenzako wote ndiyo hivyo hivyo tulipitia humo humo pale unapodhani unatenda jema asubuhi wanakuponda, ndiyo muziki wenyewe lakini mara kuna hili kuna lile saizi mimi nalala usingizi unaisha kabisa kama kuna watu wananisumbua watakuwa ni wajukuu tu" alisema Kikwete 


source:muungwana

Related Posts:

  • HASIRA:Mwanamke atafuna na kumeza $9,000 Colombia Noti za dola 100  Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES Mwanamke mmoja nchini Colombia alitafuna na kumeza pesa zote alizokuwa amejiwekea kama akiba, kuzuia mumewe asizichukue na kuzitumia. Sandra Milena Almeida alime… Read More
  • Mafuriko yasababisha shule zote kufungwa Zanzibar Shule zote katika kisiwa cha Zanzibar zimefungwa kwa muda kutokana na mvua kali ambayo imesababisha mafuriko. Waziri wa elimu katika kiswa hicho Riziki Pembe Juma amesema kuwa mvua hiyo ambayo pia imekuwa ikinyesha katika… Read More
  • Kaburi la mwana wa Pharaoh lapatikana Misri Kaburi la miaka 3,700 la mwana wa kike wa Pharaoh linaamika kupatikana karibu na mabaki ya piramidi iliogunduliwa Misri. Wizara ya mambo ya kale imesema kuwa kaburi hilo lililopo katika eneo la kifalme la Dahshur Kusini m… Read More
  • RATIBA YA LIGI YA AJUCO             AJUCSO MINISRTY OF SPORTS AND ENTERTAINMENT AJUCSO LEAGUE                     &n… Read More
  • Majaribio ya ndege mpya za Boeing yasitishwa Shirika la ndege la Boeing limesitisha kwa muda safari za kufanyia majaribio ndege yake mpya ya 737 MAX kutokana na uwezekano wa kasoro kwenye injini za ndege hizo. Hatua hiyo imechukuliwa siku chache kabla ya shirika hil… Read More

0 comments:

Post a Comment