Thursday, 18 May 2017

Rwanda yaitoza MTN faini ya dola milioni 8

Kampuni hiyo inatuhumiwa kuhifadhi data za wateja wake nje ya Rwanda kinyume na makubaliano.
Kampuni kubwa ya mawasiliano ya MTN tawi la Rwanda imetozwa faini ya zaidi ya dolla milioni 8 za Marekani kwa kile kilichotajwa kuwa kukiuka makubaliano baina yake na serikali ya nchi hiyo.
Kampuni hiyo yenye wateja takriban milioni 4 nchini Rwanda inatuhumiwa kuhifadhi data za wateja wake nje ya Rwanda kinyume na makubaliano.
Tangazo hilo linasema kuwa MTN ilikwenda kinyume na makubaliano baina yake na serikali na masharti kadhaa waliyotia saini kabla ya kupata leseni ya kufanyia kazi nchini humo
Mamlaka hayo yameishtumu kampuni ya MTN kufunja mkataba na upande wa tatu nje ya nchi kuhusu kuhifadhi data za mawasiliano za kampuni hiyo.
Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa isipokuwa taarifa kuwa hifadhi ya data hizo inapatikana nchini Uganda ikitumiwa na nchi za maeneo ya afrika ya kati na kusini.
Mamlaka hayo yameishtumu kampuni ya MTN kufunja mkataba
Mamlaka ya Rwanda ya udhibiti wa huduma za umma inasema inalichukulia kama kosa kubwa na kuitaka kampuni hiyo kulipa faini hiyo haraka iwezekanvyo kupitia benki kuu ya taifa.
Kwa upande mwingine, tangazo kutoka makao makuu ya MTN nchini Afrika kusini limeeleza kufahamishwa kuhusu faini hiyo na kwamba wataitafakari na kuendelea na mazungumzo na serikali ya Rwanda kuhusu tatizo hilo.
Hii ndiyo faini kubwa zaidi kuwahi kutolewa na mamlaka ya udhibiti wa huduma za umma nchini Rwanda.
Hii ndiyo iliyokuwa kampuni ya kwanza ya mawasilianonchini Rwanda iliyoanza shughuli zake mwaka 1998 na ambayo sasa ina wateja zaidi ya milioni 4 .

SOURCE:BBC

0 comments:

Post a Comment