Thursday, 18 May 2017

Trump aipa Tanzania $526m kukabiliana na ukimwi

Rais wa Marekani Donald Trump
Serikali ya Marekani kupitia ofisi ya rais Donald Trump imetangaza kupatia Tanzania ufadhili wa kukabilana na virisu vya ukimwi.
Marekani, ambayo siku chache zilizopita ilitangaza kusimamisha ufadhili wake kwa wizara ya afya nchini Kenya, imeipa Tanzania kitita cha dola milioni 526.
Kitita hicho kutoka mfuko wa PEPFAR, kitatumika kufanikisha mpango wa kutoa huduma kwa zaidi ya watu milioni 1.2 wanaoishi na virusi hivyo.
Akizungumza baada ya tangazo hilo, mwakilishi wa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Virginia Blaser amesema kuwa wanalenga kufanikisha kizazi kilicho huru kutoka virusi nchini Tanzania.
''Kwa niaba ya raia wa Marekani, tunafurahia ushirikiano wetu na Tanzania na tunajitahidi kuhakikisha hakuna anyeachwa nje," Alisema.
Miongoni mwa huduma hizo ni matibabu, ukaguzi, na kuzuia maambukizi mapya ya virusi hivyo kuanzia sasa hadi Septemba mwaka ujao.
Halikadhalika, serikali ya Marekani itashirikiana na serikali ya Tanzania kutekeleza huduma za kuwapima raia milioni 8.6 ili kuwawezesha kujua hali yao ya virusi.
Pesa hizo pia zitatumika kuimarisha maisha ya wajane na mayatima wa viurusi hivyo, kuzuia dhulma za kijinsia, pamoja na kuwafikia zaidi ya watu laki tatu walioambukizwa.
Mashirika mbalimbali yanayoendesha miradi mbalimbali ya afya nchini Tanzania, kama vile (TACAIDS), na wakfu wa rais mstaafu, Benjamin Mkapa (Benjamin Mkapa HIV/AIDS Foundation (BMAF)) yanatarajiwa kushiriki kufanikisha mpango huo.
Mapema mwezi huu, Marekani ilikatiza ufadhili wake wa miradi kama hivyo nchini Kenya pamoja na kuyazuia mashirika dhidi ya kufanikisha miradi yoyote na wizara ya afya ya taifa hilo kutokana na usimamizi mbaya wa fedha.
SOURCE:BBC

Related Posts:

  • Zitto njia panda uteuzi Anna Mghwira Kiongozi wa Chama Cha Act-Wazalendo hajajua cha kujibu kuhusu suala la uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama hicho  Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Zitto amesema kuwa Chama hicho kitatoa tamko baada ya Mwen… Read More
  • Uwoya astushwa na habari za Ujauzito Sexy lady wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krish’ amefungukia madai kuwa, kwa sasa ametengeneza urafiki wa muda na ndimu, samaki wabichi na ukwaju kwa kinachosemekana ni mjamzito.Huku akionesha kushtushwa na … Read More
  • PICHA: Jinsi Juventus walivyorejea kwao baada ya kipigo cha Real Madrid  Baada ya kupoteza kwa kufungwa kwa mabao 4-1 dhidi ya Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Juventus wamerejea nyumbani Italia.Pamoja na kuukosa ubingwa, mashabiki walionekana kuwapongeza wakiwapungia … Read More
  • Mataifa sita ya Kiarabu yavunja uhusiano wao na QatarHaki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMji mkuu wa Qatar, Doha Mataifa sita ya Kiarabu, zikiwemo Saudi Arabia, Misri, Bahrain, Umoja wa Milki za Kiarabu na Yemen, yamekata uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar yakiilaum… Read More
  • VIDEO:Aliyetengeneza Audio Wema na Mbowe VIDEO:Aliyetengeneza Audio Wema na Mbowe Baada ya Audio Ambayo imewekwa kwenye mtandao wa Jamii Forums Ikisikika sauti zinazosemekana kuwa ni Wema Sepetu na Freeman Mbowe Wakiongea Kimahaba Wakipanga kukutana Kwa ajili ya… Read More

0 comments:

Post a Comment