Thursday, 18 May 2017

TISA MBARONI KWA KUVUNJA NYUMBA, WIZ

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu tisa  kwa tuhuma za  kujihusisha  na uvunjaji wa  nyumba  na kuiba mali wilayani Ilemela.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Mwanza, Ahmed Msangi,  alisema watu hao walikamatwa  kutokana na   doria na msako wa watu wanaojihusisha na uvunjaji wa nyumba usiku na kuiba mali  iliyoanza Aprili 9, mwaka huu.
Alisema askari walifanya operesheni hiyo  katika   Kata ya Kirumba likiwamo soko la Kirumba, Kitangiri, Nyamanoro, Pasiansi, Ibungilo na Kawekamo wilayani Ilemela  baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
“Watuhumiwa waliokamatwa katika oparesheni hiyo ni Sandru Seleman(24) mkazi wa Ghana, Joseph Kichonge(28) mkazi wa Uhuru, Victor Sylvester (28) mkazi wa Igombe na Damali Samwel (29) mkazi wa Isenyi.
“Wengine ni Proches Samwel (20) mkazi wa Kigoto, Timoth Paul(53) na Ahmed Bajber (27)m wakazi wa Kilimahewa, Elias Samwel (35) pamoja na  Daud James(20) wakazi wa Mecco,” alisema Kamanda Msangi.
Alisema katika operesheni hiyo pia  ilikamatwa mali na vitu mbalimbali zikiwamo  runinga.
  Msangi  alisema watuhumiwa wote wanahojiwa na jeshi la polisi na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani huku msako waa kuwakamata wahalifu wengine wa aina hiyo   unaendelea.
  Kamanda aliwataka  wakazi wa Mkoa wa Mwanza  kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu mapema  waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

SOURCE:MTANZANIA

0 comments:

Post a Comment