Rais wa Marekani na Urusi wameongea
kwa njia ya simu kujadili namna ya kushughulikia migogoro mbalimbali
inayoikabili dunia kwa sasa.
Taarifa kutoka ikulu ya marekani
zinasema kuwa Donald Trump na Vladimir Putin wamekubaliana kuwa vita
vinavyoendelea Syria vimefikia katika hatua mbaya na pande
zinazohasimiana hazina budi kukaa pamoja na kumaliza mapigano hayo.Viongozi hao wawili pia wamejadili namna ya kufanya kazi kwa pamoja kuliangamiza kundi la IS pamoja na suala la nyuklia la Korea ya Kaskazini.
Haya ni maongezi ya kwanza kwa viongozi hao wawili, tokea Trump alipoishambulia Syria inayoingwa mkono na Urusi.
Source: BBC
0 comments:
Post a Comment