Utafiti mpya umebaini kwamba kerengende wa kike huwa anajifanya kuwa amekufa ili kukwepa wenzao wa kiume.
Rassim
Khelifa, kutoka chuo kikuu cha Zurich Switzerland, anasema kwamba
aliona kerengende wa kike aliyekuwa akifuatwa na wa kiume ili kufanya
mapenzi, akijiangusha na kulala kana kwamba amefariki, hadi pale
kerengende wa kiume alipoondoka.Ripoti hiyo imechapishwa kwenye jarida la ikolojia.
Bwana Khelifa amsema kuwa kerengende wa kike hunyanyaswa kwa sababu huwa hawana ulinzi baada ya kutaga mayai ikilinganishwa na kerengende wengine.
SOURCE: BBC
0 comments:
Post a Comment