Friday, 2 June 2017

Azam wafunguka Ishu ya Aishi Manula kusaini Simba

Afisa Habari wa klabu ya Azam, Jaffar Iddi amefunguka na kukanusha taarifa zinazoendelea mitaani kuwa kipa namna moja wa Azam FC, Aishi Manula amesaini mkataba na klabu ya Simba na kudai kuwa mchezaji huyo bado atabaki Azam FC.

Jaffar Iddi amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa Habari ambapo alikuwa akitoa picha jinsi klabu ya Azam itakavyoendeshwa sasa kwa kusema saizi wao watatoa kipaumbele zaidi kwa wachezaji wanaochipukia na kusema klabu hiyo saizi haiwezi haiwezi kutumia gharama kubwa sana kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma katika usajili, huku akisisitiza kuwa mazungumzo ya kuwabakisha Manula na Shomari Kapombe yapo katika hutua nzuri. 

"Nisema tu kwamba Aishi Manula, Shomari Kapombe mikataba yao inakaribia kuisha lakini mazungumzo ya Aishi Manula na Shomari Kapombe yapo katika hatua za mwisho kabisa na nisema tu yanakwenda vizuri. Aishi Manula ataendelea kubaki Azam FC kilichobaki saizi tunategemea wakitoka Misri basi tukamilishe taratibu zao na ninawatoa shaka kuwa Aishi ataendelea kubaki Azam FC hata yeye wakati anakwenda Misri na timu ya taifa aliongea na waandishi wa habari akisema "Sitatoka Azam FC labda niende nje ya nchi nikacheze lakini kwa timu za hapa nyumbani sitaweza kufanya hivyo" kwa hiyo kauli yake inaenda na kauli ya klabu ni kweli alikuwa anazungumzwa kuwa anakwenda kwenye klabu za hapa nyumbani lakini yeye mwenyewe ameweka wazi hilo" alisema Jaffar Iddi 

Mbali na hilo Jaffar Iddi amesema kikosi cha Azam FC hakitakwenda nchi yoyote ili kupiga kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara bali wao wataweka kambi hapa hapa nchini na kudai watakuwa Chamanzi, huku akibainisha kuwa wao wataanza maandalizi ya msimu mpya mwezi wa saba. 

0 comments:

Post a Comment