Friday, 2 June 2017

Kemikali za Kutengeneza Dawa za kulevya Zilivyonaswa Dar

Mamlaka ya Kupambana na Kuthibiti Madawa ya Kulevya ‘unga’, leo imekamata na kukagua kontena mbili zenye kemika zaidi ya lita 5,000 ambazo kama zikichepushwa zinaweza kutengeneza dawa za kulevya ‘unga’.

Operesheni hiyo imeongozwa na kamishna wa mamlaka hiyo, Rogers Siyanga na mamlaka zingine ambapo walivamia ofisi za AMI zilizopo Tabata jijini Dar ambao wanahusika na masuala ya mizigo.

Akizungumza na wanahabari, Kamishna Msaidizi wa Ukaguzi na Sayansi ya Jinai, Bertha Mamuya amesema kilichofanyika leo ni muendelezo wa oparesheni ambazo zimekuwa zikifanywa na mamlaka hiyo.

“Tulikuja kufanya uchunguzi kwenye hizi kontena mbili ambazo ni mali ya Kampuni ya Techno Net Scientific ya Kijitonyama, Dar. Tumebaini kuwemo kwa kikali zaidi ya lita 5,000 ambazo baadhi yake zikitumiwa vibaya zinaweza kutengeneza dawa za kulevya.

“Kama mamlaka, tutapeleka sampo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye atawasilisha kilichobainika,” alisema Mamuya.

SOURCE:MUUNGWANA

Related Posts:

  • Je unawajua wakongwe waliozoea kufanya kazi duniani?Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGESImage captionMwanamfalme Philip anasema atajiuzulu baadaye mwaka huu Wakati Mwanamfalme Philip, anayeingia miaka 96 mwezi Juni anastaafu majukumu yake ya kifalme baadaye mwaka huu, tunawaan… Read More
  • Alberto Msando ajiuzulu Ushauri wa chama cha Act-Wazalendo Mkuu wa Chama Cha Act-Wazalendo Zitto Kabwe amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa mshauri mteule wa Chama hicho Albarto Msando."Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Ch… Read More
  • Polisi 4 wauawa katika mlipuko Garissa KenyaHaki miliki ya pichaEPAImage captionMaafisa wa usalama katika shambulio la 2015 ambapo watu 147 waliuawa katika shambulio la al Shabaab dhidi ya chuo kikuu cha Garissa Kenya Maafisa 4 wa polisi wameuawa na wengine 4 kujeruhiw… Read More
  • Muungano wa wafanyakazi wampiga marufuku rais ZumaImage captionMuungano wa wafanyikazi nchini Afrika Kusini Cosatu Baraza la Muungano wa wafanyikazi nchini Afrika Kusini Cosatu ambalo ni mshirika mkuu wa chama tawala cha ANC limempiga marufuku rais Jacob Zuma kuhutubia katik… Read More
  • Manji amethibitisha tena kujiuzulu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amethibitisha kuachia ngazi katika nafasi ya Uenyekiti wa klabu hiyo, uamuzi ambao aliuchukua tangu Mei 20, mwaka huu. Kutokana na uamuzi huo wa Manji sasa Yanga itakuwa chin… Read More

0 comments:

Post a Comment