Watu wengi wanaotaka kununua simu janja/Sikanu (Smartphone), mojawapo ya jambo wanaloangalia pindi wafanyapo uchaguzi wa simu ni ukubwa wa uhifadhi wa ndani (storage).
Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kupata wasaa wa kusanidi (Install) App nyingi zaidi kadri iwezekanavyo, lakini hilo ni tofauti sana kwa Rais wa Marekani Donald Trump.
Kwa mujibu wa ripoti mpya imeelezwa Simu binafsi ya Rais wa Donald Trump imesanidiwa (Installed) App moja tu.
Mwandishi wa habari za kisiasa na mhariri wa AXIOS Media, Mike Allen, anasema Rais Trump anatumia simu ya iPhone na kwamba simu yake imewekwa App ya Twitter tu.
Sababu ya kufanya hivyo na kumuwekea App hiyo ni kupunguza hatari ya uwezekano wa simu yake kudukuliwa. Aidha pia kumpunguzia muda wa matumizi ya simu na ili ajielekeze zaidi katika mambo ya kio�si zaidi.
Muda mwingi hutumia kuangalia TV ili kujua matukio yanayoendelea duniani.
Simu ya awali ambayo alizuiwa kuitumia baada ya kuwa Rais ilikuwa ni Samsung. Alibadili kutoka Android kwenda iOS mwezi Machi mwaka huu.
Mpaka anaapishwa kuwa Rais wa Marekani inaelezwa simu aliyokuwa anatumia ni Samsung Galaxy S3 ambayo ilitolewa mwaka 2012.
Rais aliyepita Baraka Obama alisema wakati wa kuingia madarakani kwamba anatumia BlackBerry na matumizi yake yalikuwa ni kutuma ujumbe, kupiga picha na kusikiliza Muziki.
Chanzo: Teknokona
Friday, 2 June 2017
Home »
» App Pekee Iliyopo Kwenye Simu Anayotumia Rais wa Marekini Donald Trump
App Pekee Iliyopo Kwenye Simu Anayotumia Rais wa Marekini Donald Trump
Related Posts:
Kipa Mcameroon aomba Kibarua Yanga KIPA Youthe Rostand amewaambia viongozi wa Yanga SC waache kumuogopa na wamuite mezani wazungumze kama kweli wana nia ya kumsajili.Kumekuwa na tetesi za muda mrefu kwamba kipa huyo Mcameroon ambaye timu yake iliyomleta n… Read More
HATIMAYE:Niko tayari kuondoka Barcelona- Iniesta Nohodha wa Barcelona, Andres Iniesta bado ana ndoto za kuzeekea kwenye Liga ya La Liga, huku akisema kwamba iwapo atatakiwa kuondoka yupo tayari kufanya hivyo. Iniesta mwenye miaka 33 mkataba wake unamalizika katikati… Read More
PICHA: Kwa mara ya kwanza Rayvanny amempost mtoto wake na Ujumbe mzito Mwimbaji staa wa Bongofleva kutoka WCB Rayvanny leo May 31, 2017 kupitia account yake ya Instagram kwa mara ya kwanza amepost picha ya mtoto wake Jaydan ikiwa ni kumtambulisha kwa mashabiki wake. Rayvanny aliandika… Read More
Imevujaa!! Kumbe John Bocco alikuwa anahitajika Azam Golikipa namba moja wa Azam FC Aishi Manula amesema, John Bocco ‘Adebayor’ bado alikuwa anahitajika ndani ya kikosi cha Azam. Manula amesema, licha ya timu yake kusajili wachezaji wengi wa kigeni miaka ya hivi karibuni … Read More
Daktari wa upasuaji matiti afungwa jela miaka 15 Daktari wa upasuajia wa matiti Ian Paterson amefungwa jela miaka 15 kwa kufanya upasuaji usio muhimu. Paterson, mwenye umri wa miaka 59, aliwafanyia upasuaji wanawake tisa na mwanamume mmoja baada ya kuwadanganya k… Read More
0 comments:
Post a Comment