Sunday, 4 June 2017

Lowassa: Rais Magufuli anafagia fedha za Watanzania

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. Edward Lowassa amefunguka na kusema kuwa Rais Magufuli alianza vizuri kwani yapo mambo aliyoyafanya ni mazuri lakini pia yapo mambo mengine amefanya yana matatizo.

Lowassa amesema haya alipokuwa akifanya mahojiano na kusema kwa sasa tumuache Rais Magufuli aendelee na kazi yake lakini baadaye ndiyo watu waweze kumuhukumu kutokana na mambo ambayo ameyafanya.

"Rais Magufuli ameanza vizuri kubana mambo mazuri amefanya lakini kuna mambo mengine yana matatizo, lakini Mwalimu Nyerere aliwahi kusema wakati unafagia, unaweza kufagia hata shilingi sasa Rais Magufuli anafagia shilingi nyingi. Lakini tumuachie aendelee na kazi tumuhukumu baada ya kipindi fulani" alisisitiza Lowassa 


SOURCE:,MUUNGWANA

0 comments:

Post a Comment